Saturday, February 24, 2018

MAMBO YA FEDHA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

PATA SIMULIZI YA KUSISIMUA NA YENYE MAFUNZO MAKUBWA,ILIYOANDIKWA NA MTUNZI MAHIRI WA RIWAYA NCHINI;SULTANI TAMBA:-

MAMBO YA FEDHA.

Mtunzi;Sultan A.Tamba.

SEHEMU YA KWANZA.

SURA YA KWANZA.

NILIINGIA ofisini mapema kuliko kawaida.
    Ni miezi kumi na moja kamili tangu nilipopandishwa cheo na kuingia katika ofisi yenye hadhi nikiwa kama Meneja Mkuu wa Shirika la Uchapishaji,lenye makao yake makuu Dar es Salaam.Shirika la umma ambalo lilielekea kudorora vibaya baada ya kukwama kutokana na uzalishaji kuwa duni.

Mitambo kadhaa ilikufa kutokana na uzembe mkubwa uliokuwa umefanywa na uongozi uliopita,uongozi ulionekana kujali zaidi maslahi yao kuliko maslahi ya Shirika.Asilimia kubwa ya wafanyakazi walikuwa hawajalipwa mishahara yao kwa karibu mwaka mzima.

     Ndipo Bodi ilipoona haja ya kuniteua mimi,Adam Kikuku kuwa Meneja Mkuu mpya.Cheo nilichokuwa nakikililia,kiasi nikalazimika kufanya kazi kama mwendawazimu nikiwa kama ofisa mkuu wa mauzo kwa matarajio ya kuwa Bodi itaona juhudi zangu. Na kama bahati ya Mtende jangwani,niliteuliwa katika nafasi niliyoitaka.

     Rose,Katibu muhtasi wangu mpya ambaye nilibadilishiwa wiki tatu tu zilizopita,nilimkuta akifuta vumbi mashine  yake ya kupigia chapa.Sikutaka kumsemesha.Nilimsogelea taratibu,nikasimama nyuma yake.

Nilimwacha kwanza amalize.
    Asubuhi hiyo nilikuwa ndani ya suti safi nyeusi ambayo ni mara chache sana kuivaa. Ama kuwe na mikutano ya bodi, au ahadi na mrembo…..
Ndio mambo muhimu kwangu.  

      Nilitumia muda huo kumsanifu msichana huyu.Kichwani nikijaribu kukumbuka uwezo wake wa kazi na juhudi zangu mpya za kulifufua shirika kama zitalingana. Nilihitaji mchapakazi mwenzangu,ambaye tutashirikiana kwa hali na mali, usiku na mchana katika mambo muhimu ya Shirika.

     Lakini juu ya hivyo, Rose alinisisimua. Si kutokana na uhodari wake kazini tu, lakini zaidi ni umbo lake.. Alionekana anafaa zaidi kwa kazi nyingine, kuliko ofisini. Nikashangaa nilipokumbuka maneno yake kwamba alikuwa bado kuolewa, msichana mzuri kama huyu akakosa mume!

            Ana makosa gani kwa Mungu?
            Rose alimaliza kazi ya kufuta mashine yake, akageuka, kinywa kikiwa wazi kwa mshangao, aliniangushia tabasamu la kukata na shoka aliponiona nimesimama mlangoni nikimtumbulia macho.
          “ Bosi…. Mbona…. Umeingia Kimya kimya?”
          Sikujibu upesi, nilivuka kizingiti cha mlango,nikaingia.

Nini kiliendelea hapo? Tukutane sehemu ya pili….

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI