Sunday, July 20, 2014

SHINYANGA YAPIGA MARUFUKU BIASHARA YA NGONO

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

YUPO kikazi zaidi
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga;Ally Nassoro Rufunga,amepiga marufuku biashara ya ngono inayoshika kasi katika Halmashauri za Manispaa ya Shinyanga na ya Mji wa Kahama kwa kuziagiza mamlaka zinazohusika
kufuata mkondo wa sheria dhidi ya matendo hayo.

Rufunga alitoa agizo hilo katika kikao baina yake na Asasi zisizo za kiraia zinazojihusisha na mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi wilayani Kahama,ambapo alipatiwa utekelezaji wa shughuli na changamoto zinazozikabili Asasi hizo katika mapambano dhidi ya Ukimwi.




MMOJA wa wanaojiuza 

Alisema vita hivyo vya mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya Ukimwi katika  Mkoa wa Shinyanga inaathiriwa na kuwepo kwa jamii iliyojitosa kuanzisha madanguro na kufanya biashara ya ngono.

Aidha aliziomba Asasi zinazojihusisha na miradi ya mapambano ya Ukimwi zishirikiane na serikali kwa kuyafichua madanguro hayo kisha kuwapatia elimu wajihusishao na biashara hiyo kwa kuwajengea uwezo wa kujihusisha na shughuli za ujasiriamali.


AKINA dada poa wakiwa mawindoni

Alizitaka Asasi hizo ziwaunganishe machangudoa katika vikundi vya kijasiriamali huku zikifanyika jitihada za kuwatafutia mitaji hatua itakayosaidia kuondokana na vitendo vyao vya biashara ya ngono na kusaidia kupunguza maambukizi ya Ukimwi.








MKUU wa Mkoa wa Shinyanga;Ally Nassoro Rufunga,mkono wake wa kushoto anayeonekana ni Mkuu wa wilaya ya Kahama;Benson Mpesya.


“Madanguro yafichuliwe,na gesti zinazofanya na kuhamasisha biashara ya ngono zichukuliwe hatua kwakuwa wanafanya jinai,”Alisema Rufunga.


ETI wapo Ofisini wakisubiri Wateja


Awali Mkurugenzi wa miradi wa SHDEPHA+ wilaya ya Kahama,Venance Mzuka alibainisha kuwepo kwa biashara ya ngono wilayani Kahama kwa akiana dada wanaojiuza kukodi na kulipia vyumba kwa mwezi mzima katika baadhi ya Nyumba za kulala wageni.

“Kuna ongezeko kubwa la biashara ya ngono mjini Kahama kutokana na mji kukua kwa kasi,sababu ikiwa ni uwepo wa migodi mikubwa na midogo ya madini,huku gesti baadhi zikitumika ambazo siku zote tangu asubuhi utaambiwa vyumba vimejaa”,Alisema Mzuka.


YUPO mawindoni kusaka mkate wa kila siku


Mkoa wa Shinyanga hadi kufikia Juni mwaka huu ulikuwa na maambukizi asilimia 5.9 huku wilaya ya Kahama ikiwa na maambukizi asilimia 6.1 ambapo Halmashauri ya Mji ikiongoza kwa asilimia 7.8,ikifutiwa na halmashauri ya Mji wa Kahama kwa asilimia 7.8,Msalala asilimia 5.6 na Ushetu ni asilimia 5.0.

Pamoja na kiwango hicho cha maambukizi imeweka mkakati kufikia mwaka kesho 2015 uwe chini ya asilimia za kitaifa ambazo ni 5.1.


KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI