AMRI imetolewa
ya kusitisha,ujenzi wa nyumba za makazi katika Mtaa wa Igomelo,Kata ya
Malunga,Halmashauri ya Mji,wilaya ya Kahama,Mkoani Shinyanga,kutokana na baadhi
ya wananchi kushutumiwa kupoka Ardhi.
Uendelevu wa
majengo katika eneo hilo,umepigwa marufuku,kufuatia kuvamiwa na kufanyika shughuli za ujenzi, eneo la chuo cha Maendeleo
ya Wananchi(MWAMVA).
Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, William Lukuvi, jana alichukua
maamuzi hayo chuoni hapo katika Mkutano wa hadhara, baada ya kupokea malalamiko
kutoka kwa Kaimu Mkuu wa chuo cha Mwanva,Wamoja Matanza, kuwa sehemu ya eneo la
chuo hicho,limevamiwa na kujengwa nyumba za makazi.
Matanza
alisema Chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1978,mnamo mwaka 1977 kilipewa
hekari 340,na serikali ya kijiji kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kilimo ,lakini
zimebaki hekari sita baada ya kuvamiwa na wananchi wanaojenga nyumba za makazi.
Aliitupia
lawama Halmashauri ya Mji wa Kahama,kukuza mgogoro huo baada ya kushindwa
kulipima eneo hilo,licha ya Chuo hicho cha Mwanva,kufuata utaratibu na kulipia gharama za upimaji Shilingi Milioni Mbili.
“.. baada ya kupeleka maombi hayo Halmashauri ilipima
hekari 48, zilizokataliwa na aliyekuwa mkuu wa chuo hicho miaka ya nyuma,
kwakuwa zilikuwa chache na ilivyokuwa hapo awali,ndipo wananchi walipovamia kujenga
nyumba za makazi kiholela,”alisema.
Kufuatia
malalamiko hayo Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi William Lukuvi
aliamuru wananchi kusitisha ujenzi katika eneo hilo hadi hapo atakapounda tume
ya uchunguzi ni namna gani wananchi walipatiwa eneo hilo,linalodaiwa mali ya
Chuo cha MWAMVA .
Lukuvi
alisema kuwa Ofa na hati zilizotolewa na Halmashauri hazipo kihalali kwani kuna
baadhi ya hati na ofa hazikulipiwa na nyingine zikionesha kugushiwa nakuongeza
kuwa kugushi nyaraka ya serikali kwa kujipatia eneo nikosa kisheria na hao
waliogushi ofa na hati wataisaidia tume ni namna gani walipata maeneo hayo.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Anderson Msumba, alisema hati
na ofa zilizotolewa kwa wananchi waliovamia eneo la Mwamva ni batili na
kuongeza zilitolewa na Afisa ardhi mteule,aliyefukuzwa; Charles Kitalya, kipindi cha Halmashauri ya wilaya ya Kahama.
“Mheshimiwa
Waziri hati na Ofa unazoziona hapa Halmashauri yangu haihusiki nazo nawala
haizitambui zilitolewa na halmashauri ya wilaya kabla
haijagawanyika na kupatikana halmashauri za Mji,Msalala na Ushetu,mbali na
hivyo, niliisitisha ujenzi na utoaji wa ofa ama hati katika eneo hili” alisema
Msumba.
Nae
Mwenyekiti wa Mtaa wa Igomelo kata ya Malunga wilayani hapa Agustino Mabula
alisema kuwa eneo la Chuo cha Maendeleo ya Wananchi,kabla ya kupewa chuo hicho
lilikuwa likimilikiwa na kijiji nakuongeza kijiji ndio kilikuwa
kikigawa maeneo hayo kwa wananchi waliotaka kujenga katika eneo hilo hali iliyopelekea
wananchi kujenga makazi na wengine kuuza.
Hoja hiyo
ya mwenyekiti ilipingwa na Waziri Lukuvi kwa madai kijiji hakina mamlaka ya
kugawa ardhi ya serikali,isipokuwa serikali ya Mtaa kwa makubaliano na wananchi
baada ya kuitisha vikao malumu na
kuandika mihutasari na kusisitiza kuwa wananchi waliojenga kwenye eneo hilo
walijenga kimakosa.
Aidha
Lukuvi alisema hati na ofa ni nyaraka
muhimu sana ya serikali, kama pasipoti ya kusafiria na haigushiwi na mtu yoyote
na kwa aina yoyote ile,na kuonya kwa waliogushi
kujipatia maeneo kinyume na utaratibu wataisaida tume katika kutatua mgogoro
baina ya chuo hicho na wananchi wanaozunguka chuo.