M
|
bunge wa
zamani wa Jimbo la Kahama,James Lembeli, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga,Khamis Mgeja,wamedaiwa kukitesa chama chao hicho
cha zamani kwa kwa kuhusishwa
na kupanga safu za uongozi katika chaguzi za
ndani za chama hicho.
Wanasiasa
hao ambao kwa sasa ni makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo “CHADEMA”wanasadikiwa
kuhusika kupandikiza wagombea wao katika chaguzi zilizofanyika ngazi ya wila na
unaotarajia kufanyika,hivi karibuni wa ngazi ya Mkoa.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti tando hili,umebaini katika chaguzi zilizopita za Jumuiya
za CCM,na ule wa Mwenyekiti katika wilaya za Shinyanga,Shinyanga
Vijijni,Kishapu na Kahama,majina ya Mgeja na Lembeli yalitawala kwa kuhusishwa
baadhi ya wagombea kuhusika nao.
Aidha
baadhi ya Wajumbe kadhaa katika mikutano mikuu hiyo,kwa nyakati kadhaa
wamedaiwa kuonekana wakibadirishana fikra na viongozi hao maeneo mbalimbali
wilayani Kahama,hatua inayowafanya baadhi ya Wana CCM kuingiwa na hofu kubwa
mkoa wa Shinyanga na wilaya zake,kupata viongozi watakaoongoza chama hicho huku
wakiwa mapandikizi ya Mgeja na Lembeli.
Wanadai baadhi
ya Wagombea na Wajumbe kuonekana kuwa na ukaribu na wanasiasa hao,ambao
wanawatafsiri si wenzao tena tangu walipokihasi CCM Oktoba 2015,na kuhamia
CHADEMA,ni sehemu ya usaliti mkubwa unaofanyika katika kipindi hiki cha chaguzi
za chama.
“Angalia
ushahidi huu wa kimazingira,tangu Mgeja atusaliti na Lowasa kwenda
CHADEMA,maisha yake yamekuwa Dar Es Salaam,lakini tangu kinyang’anyiro cha
chaguzi zetu kuanza ametia kambi,wilayani Kahama,” Kilidai chanzo chetu ambacho
hakikupenda jina lake lianikwe hadharani.
Anasema,“Watu
hawa ambao ndani ya CCM walikuwa mahasimu,lakini wakiwa Chadema ni maswahiba
wakubwa, wanashirikiana kutupangia safu ili 2020,watupige maana mara kadhaa
wameonekana katika maeneo tofauti na makada wa CCM ambao ni wajumbe wa Mikutano
Mikuu ya wilaya na Mkoa.”
Hata hivyo
akiongea kwa simu,Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga,Haula Kachwamba,alisema japo
hawatambui watu hao lakini kutokana na uelimishaji walioufanya kwa wajumbe wa
mikutano mikuu ngazi ya wilaya,anaimani wasaliti hao hawakupenya.
“ Unajua
kazi ipo kwa wapiga kura,Mimi kura yangu ni moja,wanatakiwa wamuweke nani na
hauwezi kujua kwakuwa ni siri,lakini sidhani kuwepo mapandikizi kutokana na
uelimishaji tuliokwisha kuufanya,”alisema Kachwamba.
Kwa upande
wake Mgeja,alikana kujihusisha na kampeni za kusimika viongozi wa CCM ngazi za
wilaya,ama katika uchaguzi unaotarajia kufanyika hivi karibuni wa ngazi ya
Mkoa,bali yupo Kahama kwa ajili ya mapumziko na maandalizi ya msimu wa kilimo.
“ Unajua
nipo nyumbani kwa mapumziko na ninakutana na Watanzania wenzangu wa dini na
itikadi tofauti,kubadilishana fikra kutokana na changamoto za kimaisha zilizopo
kwa sasa,sipo kwa ajili ya chaguzi za CCM na watambue mimi kisiasa ngazi yangu
ni Taifa si Mikoa ama wilaya,”alisema Mgeja.
Nae Kada
maarufu wa CCM Mkoa wa Shinyanga,Paschal Ntare,alisema mitazamo ya Wana CCM
wenzake, juu ya miongoni mwao kuwa karibu na mashabiki ama wafuasi wa upinzani
kama ilivyo kwa Mgeja na Lembeli,ni uchanga wa kisiasa,kwakuwa si kila wakati
watazungumzia siasa bali kuna maisha nje ya siasa.
“Tuache
unafiki kinapofika kipindi cha uchaguzi kuchaguliana marafiki,mimi kada wa CCM,sitatengana
na Lembeli sababu ni ndugu yangu,wala sintomuepuka Mgeja sababu ya
Itikadi,”alisema Ntare.
Aidha;James
Lembeli,alidai Busara na Hekima kwa kipindi hiki kwa Wana CCM imetoweka,kutokana
na kuanza kupandikiza utengano kwa Watanzania kwa kigezo cha Itikadi ya
Vyama,pasipo kutambua Watanzania waliishatoka katika mfumo wa chama kimoja na
wanahitaji mshikamano ili kujiletea maendeleo ndani ya Vyama vingi.
“..wanachokiasisi
wasije kugeuza ubao kwamba kinaletwa na upinzani maana wao ni mabingwa wa propaganda,lakini
watambue wanamuasi Baba wa Taifa,ambae mwaka 1995,aliishi na mwanae Makongoro
akiwa Mbunge toka upinzani,”alisema Lembeli.
Katika chaguzi
ngazi ya wilaya zilizopita,kampeni za CCM na jumuiya zake zilitawaliwa na
majina ya Lembeli na Mgeja yaliyotumika kuwadhoofisha baadhi ya wagombea ambao
ni makada wa muda mrefu walionekana na nguvu za kisiasa ndani ya chama hicho,kuwaengua
ama kutochaguliwa huku wachache wakishinda kwa mbinde kwa madai ya kuwa karibu
na Mgeja na Lembeli.