M
|
ACHI Mosi mwaka huu,utaanza ukaguzi wa magari binafsi kwa nchi
nzima,huku ikilazimika kwa gari litakalokamilisha ukaguzi kulazimika
kulipia Shilingi
elfu tatu kasha kupatiwa Stika ya uthibitisho.
Kufuatia kuanza kwa zoezi hilo Mwezi ujao,Wamiliki wa magari
madogo watatakiwa kupeleka gari zao,katika vituo vya polisi vilivyo karibu na
makazi ama maeneo yao ya shughuli zao,kusudi yafanyiwe ukaguzi kama yanastahiki
kuendelea kuwepo barabarani.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani,Masauni amewaeleza hayo jana mbele ya Wanahabari, huku akiwaasa
askari wa barabarani kutekeleza majukumu yao kwa ueledi mkubwa .
Amesema , "Askari yoyote atakayetumia nafasi yake kutoa
stika ya gari bila kulifanyia ukaguzi na ilihali halina vigezo vya kupewa stika
nataka niwaambie kuwa huu si wakati wake, zama zimebadilika".
Pamoja na hayo Mh. Masauni aliongeza kwamba "Nataka
madereva wa pikipiki ambazo zitakamatwa na kukutwa zimesajiliwa kwa
majina ya kampuni badala ya majina binafsi wachukuliwe hatua mara moja".
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani
Tanzania, Fortunatus Musilimu alisema katika Ukaguzi wa magari madogo
utakaoanza mwezi ujao, mtu atakaekiuka na kukataa kupeleka gari lake kufanyiwa
ukaguzi atakamatwa na sheria itachukua mkondo wake.