V
|
iongozi wawili wenye mamlaka za juu katika Kampuni
ya Acacia iliyo Kampuni tanzu ya Barrick
inayomiliki kwa ubia
migodi ya dhahabu ya North Mara,Buzwagi na Bulyanhulu,wamejiuzulu.
Viongozi hao wa Acacia; Ofisa Mtendaji Mkuu na
Ofisa Mkuu wa Fedha wamechukua maamuzi hayo,tangu Alhamis,huku utekelezaji wa
makubalino baina ya Serikali na Barrick ukisubiriwa.
Kwenye
barua yake, Ofisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon amesema anataka kurudi
nyumbani Australia kusimamia masuala ya familia yake wakati Ofisa Mkuu
wa Fedha, Andrew Wray akisema amepata fursa nzuri zaidi sehemu nyingine.
“Pamoja
na uamuzi huo, wote wataendelea kuhudumu kwenye nafasi hizo wakati
wakikabidhi majukumu ya ofisi kwa warithi wao,” imesema taarifa ya
Acacia iliyotolewa leo Alhamisi asubuhi.
Kuziba
nafasi hizo, Bodi ya Wakurugenzi wa Acacia imemtangaza Peter Geleta
kuchukua majukumu ya ofisa mtendaji mkuu baada ya Gordon na Jaco Maritz
kusimamia masuala yote ya fedha za kampuni hiyo.
Wote
wawili walikuwa watendaji wa Acacia kwa muda mrefu. Geleta alikuwa mkuu
wa oganaizesheni wakati Maritz alikuwa meneja mkuu wa idara ya fedha.
“Licha
ya majukumu ya uendeshaji, Geleta atahudhuria vikao vya bodi
vitakavyofanyika mwishoni mwa mwaka huu badala ya Gordon na kuifanya
idadi ya wajumbe kuendele akubaki saba,” imesema taarifa hiyo.
Kwa
miezi miwili iliyobaki, makabidhiano ya ofisi yataendelea kufanyika
mpaka Januari Mosi, mwakani yatakapohitimishwa na uongozi mpya kuendelea
kutekeleza majukumu yake.
Oktoba
19, Serikali na Kampuni ya Barrick Gold Mine inayomiliki asilimia 63.9
ya hisa za Acacia ilitangaza makubaliano yaliyoafikiwa baada ya
majadiliano ya takriban miezi mitatu ambapo kampuni hiyo ilikubali
kutekeleza masharti yote ya sheria mpya za madini pamoja na kulipa Dola
300 milioni za Marekani wakati majadiliano kuhusu kodi yakiendelea.
Oktoba 20, Wray aliwaambia waandishi wa habari kwamba Acacia haina uwezo wa kulipa kiasi hicho kwa mkupuo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI