G
|
ari
la abiria la Nkondo,limegonga Kichwa cha Treni na kusababisha watu
wawili kujeruhiwa.
Basi
hilo lililokuwa likitokea Arusha kwenda Mwanza lilisababisha ajali hiyo eneo la
Karogho Relini katika Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo saa tatu usiku juzi barabara kuu iendayo Maganzo
wakati basi hilo lenye namba za usajiri T 693 BUW aina ya Youtong mali
ya Kampuni ya Nkondo likiendeshwa na dereva Emmanuel Warengo (34).
Kamanda
alisema katika ajali hiyo, watu wawili Ramadhani Juma (38) na Eva Brown
(29) walijeruhiwa kwa kuumia kifuani na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa kwa kupata matibabu.
Alisema
chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kutochukua tahadhari
wakati wa kuvuka barabara katika njia ya treni na alikimbia baada ya
ajali hiyo na Polisi wanaendelea kumtafuta.
Katika
matukio mengine, Polisi imefanya oparesheni na kuwakamata watuhumiwa 29
wa makosa mbalimbali, kati ya hao saba kwa tukio la ukataji panga
kikongwe mmoja aliyepo wilayani Kishapu.
Kamanda
alisema katika oparesheni hiyo walikamata pikipiki saba, mifuko ya
saruji 14, magodoro mawili, vifaa vya kupigia ramli chonganishi, vifaa
vya kufanyia uhalifu, difu 15 za matolori, mabomba 14 ya kutengenezea
pombe aina ya gongo, mashine za kuvutia maji mbili na ya kuchomelea
moja.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI