A
|
liyekuwa
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu,amekikana Chama Cha Mapinduzi
“CCM”,kwa kudai hakijamkabidhi barua yoyote ya kumfukuza uanachama kama
kinavyodai.
Nyalandu ameiambia Bongo5 kuwa ndani ya chama hicho huwa kuna utaratibu
na hawamfukuzi mtu kwa barua bali kuna kuwa na vikao vinavyohusiana na
maadili hivyo basi amesema tangu awe ndani ya chama hicho hakuna kikao
kilichowahi muita kuhusiana na masuala ya maadili.
Anasema;“Wakati
najiuzulu tarehe 30 mwezi Oktoba, nilifanya hivyo kwa nia yangu
mwenyewe na kwa uamuzi wangu mwenyewe, sikuwa nimepata barua yoyote
kutoka CCM inayonifukuza."
"Kwahiyo dhana ya kwamba kulikuwa na barua
yakunifukuza uanachama sio kweli lakini vilevile ikumbukwe kwamba mimi
sikuwa mwanachama wa kawaida,nilikuwa ni mbunge wa jimbo,pili
nilikuwa ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM."
"... na utaratibu wa chama chetu
haufukuzwi tu kwa barua huwa kuna vikao vinavyohusiana na maadili huwa
vinakaa,” amesema Nyalandu.
“Hakuna
kikao chochote tangu niwe mwananchama ambacho kiliwashawahi kuniita
kuhusiana na masuala yanayohusiana na maadili, kwahiyo mimi naona
tungejikita tu kufanya muktabari wa nchi yetu tufanye siasa za ushindani
na turuhusu watu wawe huru na tusisababishe malumbano ambayo hayana
sababu yoyote,”ameongeza.
Nyalandu
Jumatatu hii ya tarehe 30 Oktoba mwaka huu aliamua kukihama chama cha
Mapinduzi (CCM) na kujivua ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI