Sunday, October 8, 2017

ZITTO ATOA NENO BADILIKO DOGO LA BARAZA LA MAWAZIRI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



Z
itto Zuberi Kabwe,Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT -Wazalendo,  amewasilisha fikra zake kwa njia ya mtandao wa kijamii,juu ya mabadiliko madogo yaliyofanywa katika Baraza la Mawaziri.

Katika maoni yake juu ya Baraza jipya la Mawaziri lililofanyiwa mabadiliko jana, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli,Zitto ametumia fursa hiyo kutoa pongezi na ushauri.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe akiwapongeza Mawaziri hao walioteuliwa ambao wengi wao ni vijana, huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidii.

“Uteuzi wa vijana kushika nafasi za juu ni hatua nzuri, naona vijana wengi wamepewa majukumu makubwa, ninawaombea watekeleze majukumu kwa weledi mkubwa”, ameandika Zitto Kabwe.

Jana Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mpya mbili, baada ya kuzivunja baadhi ya wizara ambazo zilikuwa na vitengo vingi.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI