Sunday, October 8, 2017

MBOWE AMPA "BIG UP" RAIS MAGUFULI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO







M
wenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,amesikika
akitoa pongezi kwa Rais John Magufuli,kutenganisha Wizara ya Nishati na Madini.



Amejinasibu maamuzi ya kutenganisha Wizara hiyo,ni mapendekezo yao ya Kambi ya Upinzani,ambayo kwa takribani miaka zaidi ya saba,imekuwa ikishauri Serikali kufanya hivyo.



Mbowe amesema hayo jana Jumamosi kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda.



Alisema kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa kambi rasmi ya upinzani ilikuwa inashauri wizara hiyo itenganishwe lakini ushauri wao haukufanyiwa kazi.



"Wizara ya Nishati na Madini ni wizara nyeti mno na mara nyingi tumekuwa tukiishauri Serikali iitenganishe wizara hiyo kwani ni kubwa na nyeti ila sasa wameona ushauri wetu unafaa na kuzitenganisha," alisema Mbowe.



Alisema suala siyo nani anafaa kuwa waziri na nani hafai kuwa waziri au ukubwa wa wizara ila suala ni kuona namna gani ya kuendesha Serikali ya Awamu ya Tano.



"Magufuli ajitafakari namna anavyoendesha Serikali kwani matakwa ya viongozi ndiyo yanakuwa maelekezo ya kuendesha nchi na hata mawaziri wanafanya kazi kwa matakwa ya mtu," alisema Mbowe.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI