Wednesday, October 11, 2017

UJASIRIAMALI KUMUEPUSHA BINTI KUPATA UKIMWI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




K
atika kuhakikisha  Maendeleo endelevu yanapatikana kwa jamii inayoishi pembezoni mwa miji
nchini,asasi ya kiraia ya HUHESO Foundation, imehamasisha elimu ya utunzaji fedha.




Elimu hiyo ambayo imetimiza miaka mitatu,imeambatana  na kuwezesha uundwaji vikundi 909 vya kuweka na kukopa wilayani Kahama.

Akiongea katika Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo,kilichofanyika jana Kahama mjini,Mkurugenzi Mtendaji wa Huheso Foundation,Juma Mwesigwa,alisema upatikanaji vikundi hivyo ni zao la miradi miwili wanayoitekeleza.

Mwesigwa alisema lengo la kufundisha elimu hiyo na kuhamasisha kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ni kuwezesha wananchi kutambua na kujua namna bora ya utunzaji fedha kwa jamii zilizo mbali na upatikanaji w huduma za kibenki kwa wakati.

Alisema vikundi 699 vimeanzishwa kupitia Mradi wa Pesa kwa Wote ( PKW ),unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Care Tanzania,ambao wanautekeleza katika Halmashauri tatu zilizo wilaya ya Kahama za;Msalala na Ushetu sambamba na Halmashauri ya Kahama Mjini.


“Mradi huu unaoisha Desemba mwaka huu,ulikuwa wa miaka mitatu,lengo ni kuwafikia wanawake asilimia sabini na thelathini ya wanaume,na hadi katika robo inayoisha Juni 2017,tumefanikisha kuunda vikundi 51,”alisema Mwesigwa.


Aidha alifafanua vikundi vingine 210 vimetokana na   Mradi wa Sauti,wanaoutekeleza kwa kushirikiana na Shirika la JHPIEGO katika Halmashauri ya Ushetu,unaofanya kazi ya kuhudumia Makundi maalumu yaliyo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la HUHESO Foundation,Shija Felician,alisema jitihada za shirika lake katika kutoa elimu na kuhamasisha uundaji vikundi unasaidia kupatikana kwa maendeleo stahiki.


Aliomba Serikali kuthamini mchango huo mdogo unaofanywa na Huheso kwakuwa unarejesha nidhamu ya fedha katika jamii, na kuisaidia kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi  yanalolikabili Taifa kipindi hiki.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI