W
|
azazI na Walezi,wameombwa kuwapatia elimu ya
kutosha vijana wao huku wakiwashauri kusoma
masomo,yatakayosaidia kujipatia
ajira binafsi.
Imebainishwa ajira binafsi itakuwa
kichocheo kwa jamii kushikamana na kushirikiana katika Nyanja ya uchumi,hatua
itakayosaidia kufanikisha mikakati ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga
Tanzania yenye viwanda.
Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi wa
Taasisi ya Rocken Hill Academy inayomiliki Shule ya Sekondari ya Anderlek
Ridges,Alexander Kazimil,katika mahafali ya 9 ya shule hiyo,kwa kuikumbusha
jamii kusimamia vijana wao kupata elimu ya kutosha itakayokuwa msaada wa kupata
maendeleo.
Kazimil alisema jitihada za serikali
kufikia uchumi wa kati kwa kuwa na viwanda,zitakwama pindi vijana wakikosa
elimu ya kukabiliana na changamoto za sayansi na teknolojia,kwakuwa Tanzania ya
viwanda itajengwa na Watanzania vijana,wenye elimu ya kutosha itakayosaidia
mabadiliko makubwa ya viwanda.
Kazimil aliwahakikishia
jamii,pindi ikiwa karibu na vijana wao kwa kuwekeza katika elimu,itakayosaidia
kukabili mabadiliko ya sayansi na teknologia itakayokwenda na soko la ajira
ikiwemo viwandani,sambamba na kujipatia ajira binafsi ambazo zitakuwa vichocheo
vya kuanzisha na kumiliki viwanda vidogovidogo.
Alionya wazazi wenye uwezo kifedha
kutowekeza katika elimu kwani katika ulimwengu wa sasa pasipo kuwajengea uwezo
wa kielimu vijana wao watakuwa wanawatumbu,iza katika lindi la ufukara kwakuwa
watashindwa kushindana katika ushindani wa Kibiashara.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika
Mahafari hayo ya tisa,Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama,Richard
Kilenga,aliwakumbusha umuhimu wa wazazi katika kumuongoza mwanafunzi,kuchagua
michepuo yenye tija katika suala la ajira ili kuondokana na ombwe la kuwa na
elimu kubwa,lakini akiwa katika hangaiko la ajira.
Kilenga alisema kwa kuwa wazazi
wameshaona mengi wengine ni watumishi wa serikali wanaelewa kabisa mtoto
akisoma mchepuo Fulani ajira zake ni nyingi kuliko kumuacha mtoto akapoteza
muda kusoma elimu ambayo atahangaika nayo kutafuta kazi wakati kuna michepuo
mingi ambayo akisoma atapata ajira kwa haraka.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Anderlek Ridges,Adamu Lui,aliwaasa wazazi kushikamana na walimu kuhakikisha
vijana wao wanatimiza ndoto zao kielimu,kwa kusisitiza misingi ya nidhamu na
maadili ili kumuepusha kijana kutumbukia katika matendo mabovu.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI