Friday, October 27, 2017

MVUA BALAA DAR ZABOMOA DARAJA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




M
vua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa siku tatu mfululizo,katika mkoa wa Dar Es Salaam,zimeanza kuleta madhara katika miundo mbinu ya
barabara,kwa kubomoa daraja.

Madhara yaliyosababishwa na mvua hizo zinazoendela kunyesha kuanzia juzi mchana,ni kukatika kwa daraja la Kiluvya,linalounganisha mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.



Kutokana na daraja hilo kukatika hudumza za usafiri wa magari ya abiria, mizigo na binafsi umesitishwa na wananchi wameombwa kutumia barabara ya Bagamoyo.

Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa mbalimbali ya Kaskazini, Kati, Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu Magharibu.


Aidha, mvua hizo zimesababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam yamejaa maji zikiwamo nyumba na kusababisha uharibifu wa mali.

Adha daraja lingine eneo la Mbezi beach jijini Dar es Salaam ‘maarufu la Jeshi’ kutokea Kawe limejaa maji na inadaiwa magari kadhaa yamezama na njia imefungwa.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI