W
|
atu
wasiojulikana wameendelea kuwa tishio nchini baada ya kuwavamia Mume na
mke,wakiwa wamelala nyumbani kwao,kisha kuwashambulia kwa kuwakata
mapanga,na kusabaisha vifo vya wanandoa hao .
Wanandoa
hao walikuwa na kesi mbili za kugombea ardhi katika baraza la aridhi la
Kata ya Hunyari, Tarafa ya Chamriho wilayani Bunda.
Ofisa Tarafa ya Chamriho Boniphace Maiga, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 22, mwaka huu.
Aliwataja
waliouawa kuwa ni Magina Masengwa (61) na mke wake, Sumaye Sebojimu
(58) ambao wote ni wakazi wa kitongoji cha Kiborogota Kijiji cha
Mariwanda wilayani Bunda.
Maiga
alisema wanafamilia hao walivamiwa usiku na watu wasiojulikana na
wakiwa wamelala na kukatwa mapanga kabla ya wavamizi hao kutoweka na
kuacha maiti za watu hao ndani ya nyumba hiyo.
Maiti hao waligundulika kesho yake asubuhi na mjukuu wao aliyekuwa anakwenda shambani.
“Ofisi yangu ilipokea taarifa ya mauwaji hayo kwamba watu wawili mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga.
“Kwa
hiyo chanzo cha mauaji hayo inasadikika huenda kinatokana na mgogoro wa
shamba kwa sababu walikuwa na kesi mbili katika baraza la ardhi la
Kata ya Hunyari,” alisema Maiga.
Alisema
polisi walimkamata Nyangi Nyabirumo, mkazi wa kijiji hicho kwa
mahojiano na anaendelea kushikiliwa Kituo cha Polisi Wilaya ya Bunda.
Maiga alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.
Alisema hali hiyo inaweza kusababisha upande wa pili nao kukasirika na kulipiza kisasi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI