Friday, October 27, 2017

JAMII YAONYWA KUTOCHUKUA SHERIA MKONONI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




J
amii imeombwa kutojichukulia sheria mikononi kwa kuadhibu kwa vipigo kisha kuwaua,pindi wanapowashuku baadhi ya binadamu kutenda vitendo vya uharifu.




Imetakiwa kuwafikisha katika vyombo vya dola ili sheria ishike mkondo wake na si kuchukua jukumu la kuwaua raia wasio kuwa na hatia,pindi wanapowahisi ni wezi bila   kuwa na uthibitisho wa  kutenda kosa hilo,anaandika Tunu Herman, Mwanza.

Rai hiyo imetolewa jijini hapa na Ofisa wa Fedha wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Railway Children,Mgewa Joseph,alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza kwenye ibada ya mazishi ya vijana wanne wa mitaani waliouwawa na wananchi wenye hasira,kwa kudhaniwa  ni wezi.

Alisema tukio hilo la kusikitisha lililotokea Oktoba 15 huu majira ya saa nne usiku katika eneo la Nyashana manispaa ya Ilemela, ni la kusikitisha kutokana vitendo vilivyofanywa kutozingatia sheria za nchi,na kusababisha   tukio hilo la mauaji kuacha huzuni na simanzi kubwa kwao.

Alisema vijana hao waliouwawa walikuwa wanafanya kazi naye wakiwa chini ya Shirika hilo tangu mwaka 2014 na kuthibitisha kuwa kipindi cha uhai wao, hawajawahi kukumbukwa na tuhuma za uhalifu.
Aliwataja vijana hao kuwa ni  Issa Yusufu(21, Paulo Charles(21) na Anord Maige(17) wote wakiwa ni wakazi wa Kiloleli katika Kata ya Nyamanoro katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Meneja mradi  wa kivuko Abdallah Issa ambaye alikuwa anafanya kazi kwa karibu na vijana hao ,  alisema anasikitishwa na jinsi jamii inavyowachukuluia vijana hao wakidhani ni wahalifu pasipo kutambua kuwa ni vijana wanaojitambua na wana mipango mizuri ya maisha kwa siku zijazo.

Alitaka jamii ielimishwe juu ya umuhimu wa kuwepo kwa vijana hao na washiriki kikamilifu kwa kuwalea kwa maadili na sio kuiachia serikali, wanaharakati na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kikundi cha Mkombozi Elias Mwita ambacho kimewapoteza vijana hao kwenye tukio hilo, aliiomba serikali vijana wa mitaani ni sehemu ya watu katika jamii na wasibaguliwe kwa mauaji yasiyo na hatia.

" Wanajamii watambue tunawapenda na sisi tunahitaji kuishi kwa amani kama wanavyoishi wao”alisema.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa  Mwanza, Ahmed Msangi alisema  inadaiwa kuwa vijana hao  ni wezi  na kufafanua  jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kubaini kama ni wezi na watu wengine watakaobanika kujihusisha na mauaji hayo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Niwaombe wananchi wanapowakuta wahalifu wasijichukulie sheria mkononi na badala yake watoe taarifa kwenye vyombo vya dola ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani”, alisema.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI