Saturday, September 23, 2017

WANAJESHI WAPIGWA MARUFUKU MATUMIZI YA MITANDAO ISIYO NA TIJA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

M
kuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini,Jenerali Venance Mabeyo,ametoa onyo kwa wanajeshi
kujihusisha
kushiriki katika matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.


Ameagiza wanajeshi kuzingatia miiko na maadili ya Jeshi hilo,huku wakiepuka mienendo isiyozingatia maadili ya Jeshi hilo ikiwemo matumizi mabaya ya mitandao kwa kuwa ni kinyume na taratibu za jeshi.

Jenerali Mabeyo amesema hayo leo Jumamosi katika hafla ya kutunuku nishani  ya  Luteni Usu kwa maofisa 422 wa jeshi iliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Amesema jukumu la wanajeshi ni ulinzi wa Taifa hivyo kujiingiza katika mambo yasiyofaa ni ukiukwaji wa taratibu za jeshi hilo.

Mabeyo amewataka wanajeshi kuepuka kuliingiza jeshi kwenye siasa na badala yake wanatakiwa kuwa na uzalendo kwa Taifa lao.

“Niwasihi msimame kwenye kiapo mlichoapa leo. Wapo baadhi ya askari husahau kwa haraka na kukiuka kiapo, msifike huko. Matamshi uliyoyatoa leo yanaelekeza wajibu wako, utii, kuilinda katiba, kumtii Rais na kumtumikia.” alisema Mabeyo

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI