C
|
hama cha Demokrasia na Maendeleo (
CHADEMA ) kimedai kipaumbele chake kwa sasa katika tukio lililompata
Mwanasheria wake,Tundu Lissu,ni kuokoa uhai wa Mbunge huyo wa Singida
Mashariki.
Imeelezwa kunusuru uhai wa Lissu ni
jambo bora zaidi kuliko kukimbilia kufungua kesi juu ya shambulio la risasi.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe,amefunguka
hayo kujibu hoja za kwa nini chama hicho mpaka sasa hawajafungua kesi dhidi ya
shambulio lililomsibu Tundu Lissu.
Mbowe amesema hayo wakati akizungumza
jana na wanahabari ambapo amesema kuwa baada ya tukio la Lissu kutokea akili na
mawazo ya Chadema yalikuwa kwenye kuokoa maisha ya Lissu na wanasubiri mambo
yakiwa sawa wataangalia kufanya lolote linalowezekana kwan wakati huo.
"Kwa nini Chadema hatujafungua
kesi? Kesi unafungua kwa nani? Anayechunguza ni nani? Chadema tumeshafungua
kesi nyingi ya akiwepo Ben Saanane msaidizi wangu aliyepotea kusikojulikana,
Kesi ya nyani unapeleka kwa Tumbili. Priority yetu sisi ni kumuokoa Lissu na
siyo Kesi. Kupigania maisha yake ndicho kitu tuliona kinachofaa kufanywa na
ndicho tunachofanya mpaka sasa", amesema.
"Ninaamini tu mambo yakikaa sawa
vichwa vyote hivi vya Chadema vitajua kama tunaweza kufungua kesi au kitu gani
kingine ambacho kinafaa kufanywa endapo tu afya ya Mh. Lissu
ikishaimarika" ameongeza
Akizungumzia kwanini mpaka leo dereva
wa Lissu hajarudi nchini ili kwenda kuripoti polisi kama jinsi jeshi la polisi
lilivyoagiza, Mbowe amesema kwamba kijana huyo atarudishwa nchini pindi tuu
wataalamu wa afya wanaomhudumia wakitoa ripoti afya yake kama iko salama na wao
hawapo kwa ajili ya kumficha.
"Wiki iliopita nilisema dereva wa
Mh. Lissu yupo Nairiobi kwa ajili ya matibabu ya kisaikolojia. Hatukuona kama
ni busara kumtelekeza wakati alikuwepo kwenye matatizo na boss wake. Madaktari
wakituthibitishia kuwa yuko timamu atarudi nchini kwani hatuko kwa ajili ya
kumficha mtu. Yule kijana ni kama mtoto wa Lissu, dereva na mlinzi wake, wana
miaka mingi pamoja tangu Lissu anagombea ubunge kwa mara ya kwanza"
amesisitiza.
Ameongeza pia dereva atakuja
kuzungumza nini kilitokea na yeye alijiokoaje naamini aliyekuwa anashambulia
alikuwa hajalenga kumuacha hai mtu hata mmoja hivyo mimi siyo msemaji sana wa
dereva wake Lissu lakini akipona ataelezea mwenyewe kila kitu
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI