Saturday, September 23, 2017

RAIS MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI WANAJESHI 422

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


R
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,amewatunuku kamisheni maafisa 422 wa Jeshi.




Kamisheni hizo,amezitunuku kwa Wanajeshi,ambao wamehitimu mafunzo mbali mbali kwenye chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha.

Tukio hilo ambalo limefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Mjni, limehudhuriwa na viongozi mbali mabali wa kitaifa na mafisa wa Jeshi nchini pamoja na wananchi mbali mbali wa mkoa wa Arusha.

Kabla ya kuwatunuku kamisheni maafisa hao wa jeshi, Rais Magufuli alikagua gwaride maalum, na kutoa zawadi kwa maafisa wa jeshi watano waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.

Tukio hilo la Rais Magufuli kuwapa Kamisheni Maafisa wa Jeshi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni la kwanza kufanyika katika uwanja wa wazi badala ya viwanja vya jeshi wilayani Monduli.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI