R
|
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu, Dkt. John Magufuli ametangaza nafasi za
kujiunga Jeshi kwa vijana
Elfu Tatu.
Tangazo hilo litahusisha vijana waliopitia mafunzo ya
ukakamavu kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza baada ya kuwatunuku nishani ya Luteni Usu maofisa 422 wa
jeshi, Magufuli amesema lengo la kutoa nafasi hizo ni kuhakikisha jeshi
linakuwa na askari wa kutosha.
“Jeshi haliwezi kuwa na maofisa tu, tutaongeza na askari wa kawaida,
natangaza rasmi kuwa, nitaajiri wanajeshi 3,000, nitazingatia
waliohitimu vyema mafunzo ya JKT, tunataka tujenge jeshi la kisasa.”
alisema Magufuli na kuongeza.
“Kuna mmoja alikuwa anasema habari za Jeshi tukamkamatia Mbeya
tukampeleka jeshini akajifunze kuwa msemaji wa jeshi. Wakati nateua
Wakuu wa Mikoa Wanajeshi watu waliongea, lakini mimi napenda wanajeshi
sababu mambo yao yanakwenda haraka.”
Rais Magufuli amewataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa jeshi na vyombo
vingine vya ulinzi na usalama ili viendelee kufanya kazi yao kwa
ufanisi, amani na utulivu viendelee kutawala nchini.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI