V
|
ita
vya maneno vimezidi kushika kasi baina ya mataifa makubwa ya
Marekani na Korea
Kaskazini,baada ya Viongozi wa mataifa hayo,kuzidi kurumbana.
Marumbano hayo kwa Viongozi wa Mataifa hayo,yamefikia hatua ya kukashifiana,kwa kila mmoja kumuona mwenzake hamnazo.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa matamshi ya rais wa
Marekani Donald Trump aliyemtaja kuwa ''na matatizo ya kiakili''
yamempatia motisha zaidi ya kuendelea kutengeza makombora ya taifa lake.
Katika taarifa ya kibinafsi isio ya kawaida, bwana Kim amesema kuwa rais
Trump ''atalipia kauli'' zake za hotuba ya baraza la Umoja wa mataifa
ambapo alionya kuiangamiza Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika
kujilinda.
Bwana Trump naye alijibu akisema kuwa ''mwenda wazimu'' hajawahi kufanyiwa atakachofanyiwa akijaribu.
Mataifa hayo mawili wamejibizana kwa kurushiana maneneo makali katika siku za hivi karibuni.
Rais Kim alimaliza taarifa yake kwa kusema kwamba atamnyamazisha kiongozi huyo ''aliye na akili punguani'' kwa vita.
''Pande zote zinafaa kujikaza badala ya kuchokozana'' , alisema msemaji
wa waziri wa maswala ya kigeni Lu Kang.Urusi pia ilitoa wito wa
kuvumiliana .
Msemaji wa ikulu rais Dmitry Peskov alisema kuwa Moscow ina wasiwasi kuhusu kiwango cha wasiwasi kinachozidi kuongezeka.
Korea Kaskazini imekuwa ikifanyia majaribio makombora yake katika
kiwango kisicho cha kawaida na kufanya jaribio lake la sita la kinyuklia
licha ya shutuma za kimataifa.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Korea Kaskazini Ri Yong -ho ambaye
awali alikuwa ameifananisha hotuba ya rais Trump kama ile ya ''mbwa
anayebweka'' ameonya kuwa Pyongyang italifanyia jaribio bomu lake la
H-Bomb katika bahari ya pacific kujibu tishio la rais Trump.
''Bomu hilo litakuwa bomu lenye uwezo mkubwa kuwahi kurushwa katika
bahari hiyo ya pacific'' , Bwana Ri alisema akinukuliwa na shirika la
habari nchini Korea Ksakzini Yonhap.
Hatahivyo, aliongezea: Hatujui ni hatua gani zitachukuliwa na rais Kim jong-un
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI