Saturday, September 23, 2017

FISI AIBUKA HOSPITALI KAHAMA NA KUZUA TAHARUKI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO






S
iku chache baada ya Wanakijiji wa Kakebe,Kata ya Nyandekwa kuingiwa hofu ya kuliwa fisi,aliyevamia na
kula kuku 41,hali hiyo imejitokeza tena Mjini Kahama,baada ya Fisi mmoja kuonekana akirandaranda ndani ya eneo la Hospitali ya Wilaya.



Katika tukio hilo lisilo la kawaida lilisababisha kuibua taharuki kubwa kwa wagonjwa na watu waliokuwa katika hospitali ya Mji wa Kahama,huku likizidisha Hofu ya wananchi katika maeneo mbalimbali  juu ya kuibuka kwa Wanyama wa aina hiyo katikati ya Mji,anaandika Salma Kipara.

Akizungumza na Wandishi wa Hospitalini hapo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dr. Lucas David alisema tukio hilo lilitokea jana,majira ya saa 12 alfajiri kwa Fisi huyo ambaye hakujulikani alipotokea, kufaulu kuingia ndani ya hospitali hiyo.

Alisema kuwa licha ya eneo la Hospitali hiyo kuwa na uzio  mkubwa,fisi huyo alifaulu kuingia kupitia upande wa  chuo cha Manesi ambapo kuna tundu  linalopitia karibu na chumba cha kuhifadhia maiti.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi  wa Hospitali hiyo, Dkt. Fredirick Malunde alisema baada ya kuonekana kwa mnayama huyo walitoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji,ambaye naye aliwaarifu watu wa Idara ya Maliasili ambao walifanikiwa kumuua fisi huyo kwa kumpiga risasi tatu.

“ Hali hii sasa inatisha mjini kwetu,si kawaida,tumejawa na hofu,tunatafakari usalama wetu hasa kwa watoto wetu ambao hulazimika asubuhi kwenda Shule,tuna maswaali yasiyo na mjibu juu ya wanapotoka fisi hao,”alisema mkazi wa Kahama mjini,Aidan Mwahengera.

Tukio la fisi huyo linakuja siku moja baada ya taarifa kuwa kundi la Fisi limevamia na kukatakata mabomba ya maji ya Mradi wa Kilimo cha Mbogamboga wa Kikundi cha Songambele katika kata ya Nyandekwa Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Kabla ya hapo,katika Kata hiyo iliyo katika Halmashauri ya Mji wa Kahama,Fisi,alivamia nyumbani kwa  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ihashi kijiji cha Kakebe,Daudi Martini,  na kufanikiwa kula kuku 41 kati ya 60.

Hata hivyo Katibu tawala wa Wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya,aliwatoa hofu wakazi wa wilaya ya Kahama kushambuliwa na wanyama hao kwa kudai tayari Serikali wilaya imetoa agizo kwa Halmashauri ya Mji wa Kahama,kushughulikia suala hilo  na tayari utekelezaji umeanza kufanywa na Maafisa wa Idara ya wanyama pori.



KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI