H
|
OFU imetanda kwa wakazi wa Kijiji cha
Kakebe,wilayani Kahama,juu ya kuliwa Fisi,kutokana wanyama hao
kudaiwa
kurandaranda nyakati za jioni hadi usiku hata kuvamia kwa
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ihashi kijijini hapo,Daudi Martini, na kula
kuku 41 kati ya 60.
Kutokana na tishio la Wanyama hao,
serikali ya kijiji hicho imewataka wananchi kuacha mara moja kuchota maji
nyakati za usiku kwa hofu ya kuliwa na fisi,anaandika Salma Kipara.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Daniel Mabula,ametoa
agizo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo
kwa lengo la kujionea uharibifu uliofanywa na mnyama huyo katika familia ya
mwenyekiti wa Kitongoji cha Ihashi.
Mwenyekiti huyo alisema baada ya
fisi kuvamia banda na kufanikiwa kula kuku 41,walitoa taarifa ngazi
mbalimbali zinazohusika wilayani Kahama,huku wakitoa onyo kwa wananchi
kutochota maji visimani nyakati za usiku licha ya kuwepo uhaba wa maji safi na
salama.
Tabu Katoto shuhuda wa tukio hilo anasema
licha ya wananchi kuokoa mifugo mingine pamoja na maisha ya familia hiyo
serikali inapaswa kulichukulia uzito suala hilo kwani wanyama hao wamekuwa
wakilandalanda mitaani na kuhatarisha amani.
Naye shuhuda mwingine wa tukio,
Michael Shuiyili, alisema wanyama hao wanajihifadhi katika pori
lililojirani na kijiji,hivyo kuiomba serikali kupitia idara ya wanyama pori
ifanye msako,kabla wanyama hao hawajafanya uharibifu mkubwa.
“… kwani huku kunashida ya maji fisi
atakula wake zetu wanaoenda kulinda maji usiku,” alisema Shuiyili.
Naye mwanamke mmoja aliyejitamburisha
kwa jina moja la Veronika alisema pia mnyama huyo alikula mbwa wake
mchana kweupe na alishuhudia pia ngombe mkubwa kwa jirani yake akiliwa na fisi
hao.
Kwa upande wake Katibu tawala wa
Wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya,alikiri kuwepo kwa wanyama hao na kusema kuwa
tayari Serikali wilaya imetoa agizo kwa Halmashauri ya Mji wa
Kahama,kushughulikia suala hilo na zoezi la msako juu ya wanyama hao
litaanza mara moja kwa kushirikiana na idara ya wanyama pori.