N
|
i ukatiri na unyama wa hali ya
juu,baada ya
mwanamke wa kabila la Kisukuma,Zena Mohamed (28),kumuua mme wake
Bakari Salehe (35); Mzaramo,kwa kumchinja na kisu shingoni upande wa kushoto.
Inaelezwa kuwa wanandoa hao walikuwa
wamegombana,ndipo mke akamsubiri mmewe alale ndipo alipoteleza unyama wake huo
kwa kumchoma kisu tumboni na shingoni,anaandika Salma Kipara.
Tukio hilo limetokea Septemba 20,2017,saa
mbili na nusu usiku katika kitongoji cha Malenge kijiji cha Jomu,Kata ya Tinde,Tarafa
ya Itwangi,wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema,“Baada ya kutekeleza tukio hilo,mwanamke huyo alifungua
radio kwa sauti ya juu kisha kufunga mlango kwa kufuli na kuondoka kukimbilia kwa
mama yake mzazi anaeishi Shinyanga Mjini.
“…..alipofika
akamwambia mama kuwa amefanya mauaji,hali iliyomfanya mama atoe taarifa polisi
na kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa”.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa
wa Shinyanga,ACP Haule amesema tukio hilo limetokea wakati wanandoa hao
walipokuwa wanapigana katika ugomvi uliotokea nyumbani kwao.
“Chanzo cha
tukio hilo ni wivu wa mapenzi baada ya mke kupokea simu ya mume wake iliyokuwa
ikiita na kisha kusikia sauti ya mwanamke mwingine na kuhisi kuwa ni hawala wa
muwe wake,ndipo ugomvi ulipoanzia”,ameeleza Kamanda Haule.
Kamanda huyo wa polisi amesema
wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na ametoa wito kwa wananchi
kujiepusha na kuachana na vitendo vya dhana ya wivu wa kufikirika.
“Tuache
kufikiri kuwa mwanaume akiongea na mwanamke au mwanamke akiongea na mwanaume
kwa njia ya simu au njia ya kawaida lazima kuna mahusiano ya kimapenzi,jambo
ambalo siyo kweli hasa kutokana na masuala ya utandawazi katika dunia hii ya
leo”,ameeleza Kamanda Haule.