Sunday, July 2, 2017

TAIFA STARS KIBARUANI LEO NA BAFANA BAFANA,TAMBUA MUDA KAMILI WA MECHI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




T
imu ya Taifa ya Tanzania;Taifa Stars Itaingia kibaruani leo kusaka tiketi  ya kuingia Nusu Fainali
ya Michuano ya COSAFA,kwa kuingia Dimbani  nchini Africa Kusini Kumenyana na Mabingwa watetezi wa Michuano hiyo,Timu ya Taifa ya Afrika Kusini,Bafana Bafana.


Bafana Bafana,ambao ni wenyeji wa michuano hiyo,wana matumaini kibao ya kuibuka na ushindi,kutokana na kuwa na faida ya kucheza nyumbani,hata hivyo Taifa Stars,ambao katika michuano hii imeonesha uhai,kutokana na soka wanalotandaza ambalo liliwawezesha kuongoza kundi lake na kukata tiketi ya kucheza robo fainali hii.

Mechi Hiyo Itaanza Saa kumi na Mbili Jioni (1800 hours) muda wa Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa Mechi ya Mwisho Timu hizi Kukutana,  Ilikuwa 14/5/2011 katika dimba la Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Tanzania.Katika Mechi hiyo iliyokuwa ya Kirafiki Tu Taifa Stars Ililala kwa bao 1 kwa 0, Goli la Wageni Afrika Kusini Lilifungwa dakika ya 44 na Mchezaji Siyabonga Sangweni.

Hata hivyo katika pambano la leo,Taifa Stars itakosa huduma za Wachezaji Abdi Banda na Mbaraka Yusuph,kwa sababu za majeruhi na kadi mbili za njano.

Mchezaji Abdi Banda  Atakosa Mchezo kati ya Taifa Stars na Afrika Kusini katika Robo Fainali ya Cosafa 2017,Banda anakosa kutokana na kuwa na Kadi Mbili za Njano. Mwingine atakayeukosa Mchezo wa Leo ni Mbaraka Yusuph ambaye Ni  Majeruhi.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI