R
|
ais wa Marekani, Donald Trump,amechoshwa na kiburi
cha Korea Kaskazini cha kuendelea kurusha makombora,kinyume
cha taratibu za
Umoja wa Mataifa.
Amesisitiza kwamba muda wa kimkakati wa uvumilivu
kwa Korea Kaskazini umekwisha.
Katika
hotuba ya pamoja juzi, akiwa na mwenzake wa Korea Kusini, Moon Jae
katika bustani ya Rose kwenye Ikulu ya White house, Trump aliahidi
‘kuchukua hatua madhubuti’ dhidi ya programu ya nyuklia na makombora ya
Korea Kaskazini akisema vitisho vyake vinafaa kupatiwa majibu ya
kijasiri.
“Hizi si zama za kuvuta subira juu ya Serikali ya Korea Kaskazini ambayo imeshindwa kutekeleza wajibu wake,” alisema Trump.
“Imechukua miaka mingi na imeshindikana, na kwa kweli hakuna kuvuta subira hivi sasa.”
Hata hivyo, Trump amesema ni muhimu kuwe na ushirikiano katika kugawana mzigo wa kuhakikisha usalama.
Kadhalika,
Rais wa Korea Kusini amesema kwamba Taifa lake litaweka marekebisho ya
kiusalama na kujenga msingi dhabiti wa kujikinga.
Kiongozi huyo ameshauri kuwa ni muhimu kuendelea na majadiliano na viongozi wa Korea Kaskazini.
Trump
na Moon walitofautiana jinsi wanavyotakiwa kuweka shinikizo juu ya
Korea Kaskazini ili iweze kuacha kabisa programu yake ya nyuklia.
Wakati
hayo yakiendelea, Korea Kaskazini imeendelea kushikilia msimamo wake wa
kufanya majaribio ya makombora ya kinyuklia, huku ikiongeza ubora zaidi
wa makombora yake na kudai kuwa yanafika katika kona nyingi za dunia
ikiwa ni pamoja na sehemu ya Marekani.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI