
R
|
ais John Magufuli amevutiwa kwa jinsi Watanzania walivyoingiwa
na mwamko,wa kuchangia mapato ya
serikali yao kwa kujitokeza kwa wingi kulipa
kodi za Majengo.
Amedai Watanzania wamehamasishana na kujitokeza
kwa wingi,kulipia kodi ya majengo,yao pasipo kusukumwa jambo ambalo linastahili
kupongezwa.
“Walipochukua TRA, sasa waliwathaminishia kodi ambayo wananchi wanaweza kuilipa, ndiyo maana wakajitokeza kwa wingi. Haijapata kutokea wananchi wakataka kulipa kodi kwa kiasi kile, ni kwa sababu ilikuwa nafuu kwao,” amesema
Pia, Rais amewataka TRA kuendelea kukusanya kodi kwa njia ambazo ni rafiki kwa kuwa wananchi hawapendi kodi inayowaumiza bali kodi ambayo ni sahihi kwao.
“Wananchi wanapenda kulipa kodi lakini iwe na manufaa kwao,” amesema Rais Magufuli.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI