Mosha
alisema kwa sheria ya sasa, mfanyabiashara atatakiwa kumiliki duka moja
tu tofauti na ilivyokuwa awali mtu mmoja anaweza kumiliki maduka hata
matano.
Aidha,
alisema wafanyabiashara wa Daraja B watafanya miamala ya papo kwa hapo
pamoja na miamala ya nje ya nchi. Hata hivyo, Mosha alisema mbali na
masharti ya mtaji, watahitajika pia kufunga kamera tatu ‘CCTV‘ kwa ajili
ya usalama.
Alieleza
kuwa lengo ni kudhibiti ubadilishaji wa fedha na utoaji wa stakabadhi,
kamera zinatakiwa kufungwa kaunta, kwenye kabati la kuhifadhia fedha na
eneo la kuhudumia wateja.
Alisema
watakaokamilisha masharti hayo ndio watakuwa wanaendesha biashara hiyo
kuanzia Septemba mwaka huu Wafanyabiashara hao wa maduka ya kubadilisha
fedha za kigeni wamepewa miezi mitatu kuanzia Juni 2, 2017 hadi Septemba
mosi, mwaka huu wakamilishe usajili na kumiliki duka moja tu.
Hivyo imetoa waraka kwa wafanyabiashara wa maduka ya
kuuza na kununua fedha za kigeni kuomba upya leseni kwa ajili ya kufanya
biashara hiyo. Leseni zote za maduka ya kubadilisha fedha za kigeni
zitafutwa ifikapo Septemba 2, mwaka huu ili wamiliki waombe upya.
Ofisa Msimamizi Maduka ya Kuuza na Kununua Fedha za
Kigeni wa Benki Kuu ya Tanzania, Kanuti Mosha,alisema hayo jana,kwenye Maonesho ya 41 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kwenye
Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, Temeke jijini Dar es
Salaam.
Alisema sambamba na kutoa leseni upya, BoT imeweka viwango vipya
vya mtaji ambavyo vinaanzia Sh milioni 100 hadi 300 kwa daraja A, na
kuanzia Sh milioni 250 hadi Sh bilioni moja kwa daraja B na Amana ya
Thamani kuanzia Dola za Marekani milioni 50 hadi milioni 100.
Mosha
alisema endapo mfanyabiashara atataka kufungua tawi, itamlazimu kutuma
maombi BoT.