O
|
ngezeko
la Shilingi 40 katika kila lita moja ya Mafuta ya Taa,Petroli na Dizeli
lililofanywa katika Bajeti ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka
2017/2018,imebashiriwa kwa kiwango kikubwa kushusha uzalishaji wa zao la
Mpunga.
Katika
Bajeti hiyo iliyowasilishwa hivi karibuni na Waziri wa Fedha,Dk.Philip
Mpango,ambayo imefuta leseni ya Magari na tozo hiyo kuhamishia katika ongezeko
hilo la mafuta,limedaiwa ni mwiba mchungu kwa mkulima wa Tanzania,hususani wa
zao la Mpunga,anaandika Shaban Njia.
Afisa
Uendelezaji wa masoko kutoka Baraza la Mchele Tanzania Godfrey
Rwiza,alibainisha hayo wakati wa kikao
cha wadau wa mnyororo wa thamani wa zao la mpunga kutoka Kanda ya Ziwa,kwa
kusema ili mkulima wa mpunga afikie malengo serikali inatakiwa kuliangalia
suala la ongezeko la shilling 40 kwa kila lita moja ya mafuta.
Rwiza
alisema ongezeko hilo lililofanywa halitamsaidia mkulima wa zao la mpunga
katika kuongeza thamani ya zao lake,hasa kwakuwa tayari anawajibika katika
kuchangia asilimia 24 katika bajeti ya Serikali,hivyo walistahili kupewa
kipaumbele katika kuwasaidia ili wapate kuboresha kilimo chao zaidi na si
kuwakandamiza kwa ongezeko hilo la asilimia 40.
Alisema
kuelekea uvunaji na utayarishaji wa mashamba kwa msimu ujao wa
kilimo,umewaogofya wakulima wengi ambao wamejikuta wakipaki matrekta ya kulimia
mashamba,mashine za kuvunia mpunga kwa kuogopa
ongezeko hilo.
Anasema,
“..kutokana na hali hiyo haitashangaza,kuona wakulima wakirejea kuanza kutumia
mfumo wa uvunaji wa kizamani ambao huwa unaacha mpunga mwingi shambani bila
mkulima kutambua,kwakuwa hatamudu kugharama za ununuzi wa mafuta.”
Alisema
Tanzania inazalisha mchele kwa asilimia 70, ikiwa ya pili katika ukanda wa
Kusini mwa Jangwa la Sahara,huku dunia
ikitambua mchele mzuri hupatikana
nchini,hivyo serikali ingefanya jitihada za kumsaidia mkulima kusudi
aendelee kuzalisha mchele mwingi kwa kuvuna kisasa,pasipo kubakisha mpunga
shambani ili Taifa lizidi kunufaika Kimataifa.
Nae
Mwakilishi kutoka Jukwaa la Taasisi zisizo za kiserikali zinazofuatilia bajeti
ya Tanzania(FORUMCC), Jonathan Sawaye,alishauri serikali kufungua milango ya
wafanyabiashara wa mchele kuuza mazao hayo nchi za nje hali ambayo itafanya bei
kuwa chini na kumfanya kila Mtanzania kumudu gharama za maisha.
Alisema
kuwa hapo awali kilo moja ya mchele ilikuwa ikiuzwa shilling 900 hadi 1100
lakini kwa sasa Watanzania wananunua kilo moja ya mchele shilling 2000
nakuongeza kuwa serikali kuzuia wakulima na wafanyabiashara kuuza mchele nje ni
kufanya bei kuongezeka na kuwa ghali kwa Watanzania kumudu maisha.
Kwa upande
wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhiri Nkurlu ambae alikuwa mgeni rasmi katika
warsha hiyo ya wadau wa mnyororo wa thamani wa zao la mpunga kutoka kanda ya
ziwa,alisema serikali inatambua uwepo na umuhumu wa wakulima wa zao la mpunga
kwa kuchangia asilimia 24 ya bajeti ya nchini.
Alisema
kuwa serikali ya awamu ya tano ipo bega kwa bega katika shughuli za ukuaji wa
kiuchumi hasa katika sekta ya kilimo na kuongeza kuwa wakulima kwa
ujumla,wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki ambacho serikali inafanya
tathimini ya wingi wa hali ya chakula na pindi itakapotoa majibu itaweza
kuwafungulia masoko na kuuza nchi za nje kama ilivyo ada.
Hata hivyo
Nkurlu amewataka wafanyabiashara hao kufungua viwanda vidogo vidogo vya kukoboa
mpunga ili kufungua fursa ndogo ndogo za ajira kwa vijana wanaozunguka hovyo
mitaani bila kufanya kazi hali ambayo itasaidia kupunguza wimbi la watoto wa
mitaani.