M
|
shambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo
Ngoma amezima tetesi kwamba anataka
kujiunga na Simba,baada ya
jana kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC.Ngoma mwenye miaka 27,usajili wake ulitawaliwa na tetesi za kujiunga na watani wa jadi wa Yanga,Wekundu wa Msimbazi,Simba Sport Club hhuku zikitawaliwa na kusaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Polokwane City ya Afrika Kusini.
Hii
ni awamu yake ya pili wa miaka miwili kuichezea Yanga,ambapo katika miaka yake
miwili ya kwanza, Ngoma alikuwa ana msimu wa kwanza mzuri Yanga SC, akiiongoza
kutwaa mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na
Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup
(ASFC).
Katika
michuano ya Kimataifa,aliiwezesha pia kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la
Shirikisho Afrika, baada ua kutolewa 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
Hata hivyo, msimu wake wa pili Ngoma hakuwa mzuri Yanga kutokana na kusakamwa na maumivu ya goti, huku timu yake ikiweza tu kutetea taji Ligi Kuu na kuvuliwa mengine ya Ngao ya Jamii iliyochukuliwa na Azam na ASFC lililobebwa na Simba.
Pia katika michuano ya Afrika, Yanga haikuweza kurudia mafanikio yake ya msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi.
Ngoma aliyezaliwa Kwekwe, Zimbabwe alijiunga na Yanga SC mwaka 2015 akitokea FC Platinum ya kwao, aliyoanza kuichezea mwaka 2012 akitokea Monomotapa United iliyomuibua mwaka 2011.
Amewahi kuitwa timu ya taifa ya Zimbabwe mara kadhaa tangu mwaka 2011na hadi sasa amecheza mechi nane na kufunga mabao matatu. Na kwa kusaini Yanga, maana yake ataendelea kufanya kazi na rafiki zake, kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko na mshambuliaji Mzambia, Thabani Kamusoko.