PAMOJA na vitendo vya Ukatili wa
kijinsia kukithiri huku ikidaiwa wanaume ndio vinara wa matendo hayo,lakini
imebainika Wilayani Kahama kuna wanaume wanaofanyiwa ukatili wa
kijinsia na wake zao, lakini wanaogopa
kuripoti Polisi kwa kuhofia
kujidhalilika.
Wanashindwa kufika katika
kituo cha polisi mjini Kahama kuripoti vitendo wanavyofanyiwa na wake zao kwa
hofu ya kujidhalilika kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuogopa kuachika kwa wake
zao,gazeti
hili tando la Lifali,linaeleza.
Jeshi la Polisi kitengo cha dawati
la jinsia na watoto,wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, lilinabainisha kwamba
kuna baadhi ya Wanaume ni waathirika, lakini hawaripoti vitendo
wanavyofanyiwa na wake zao kwa hofu ya kujidhalilisha.
Mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia
Wilayani hapa,Koplo Ninaely Kisagase,aliyasema hayo wakati alipotembelewa na
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu,katika banda lake la maonyesho siku ya
maadhimisho ya nenda kwa usalama barabarani.
Kisagase akiwa katika viwanja vya
CDT mjini Kahama, ambako maadhimisho hao ya nenda kwa usalama barabarani
yalifanyika Kimkoa,alimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa wapo wanaume
wanaofanyiwa vitendo vya kikatili na wanawake zao lakini wanashindwa kuwaripoti
polisi kwa kulinda heshima na ndoa zao.
Alimuhakikishia Mkuu wa wilaya kuwa
Jeshi la Polisi, linafanya kazi kwa ufanisi na usiri mkubwa,hivyo kuwaomba
wanaume watoe taarifa katika kitengo cha dawati la Jinsia na watoto,ambapo
wataketi pamoja na kuwashauri,katu hawawezi kuharibu ndoa.
“Na kama mwanaume atashindwa
kumripoti Polisi mke wake anaweza kuathirika kisaikolojia jambo ambalo ni
hatari sana kwa familia na jamii inayomzunguka na vitendo hivyo kama
vitagundulika kufanywa kwa makusudi tutafungua jalada na kuwapeleka Mahakamani
kwa sharia zaidi.
.”Aliongeza Kisagase.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kahama Fadhil Nkurlu alilitaka jeshi la polisi kuhakikisha linazidi kuimarisha
hali ya usalama ndani na nje ya Wilaya ya Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa
ujumla na kuwataka kutomfumbia macho raia yoyote anayevunja sheria za nchi
zikiwamo za barabarani.
Pia alilitaka jeshi la Polisi
kitengo cha usalama barabarani kutochukua rushwa kwa wavunja sharia barabarani
hali ambayo itasaidia kupunguza ajari barabarani pamoja na kuondokana kwa
mazoeya mabaya baina ya askari na madereva
Hata hivyo mkuu huyo wa Wilaya
alilitaka jeshi la polisi kudhibiti vitendo viovu vya madawa ya
kulevya,Viroba,mirungi na bangi na kuongeza kuwa madereva wanapotumia virevi
hivyo husababisha wajione wako sahihi barabarani japokuwa wamekiuka sharia
hizo.
Anasema;“Ajari nyingi zinazotokea barabarani
zinasababishwa na jeshi la polisi kwa kitendo cha kuchukua rushwa kwa
waliovunja sheria za usalama barabarani."
"...acheni kuchukua hizo rushwa hali hiyo
itasaidia kupunguza mazoea mabaya baina yenu Askari na watumia barabara,na
ikumbukwe sheria ya jeshi la polisi inakataza polisi kujihusisha na kupokea
rushwa ama kutoa rushwa”,alisema Nkurlu.