TAASISI
ya kuzuia na kupambana na Rushwa( TAKUKURU) Mkoa malumu wa Kahama,unalia
kushindwa kesi kunatokana na jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya kutoa ushahidi
Mahakamani.
Wananchi
wamekuwa na tabia ya usaliti kwa TAKUKURU, katika suala la kujitoa kuwasilisha
ushahidi,hivyo kusababisha kushindwa
kwa kesi nyingi zinaikabili Taasisi hiyo,anaandika
Shaban Njia.
Imedaiwa
Wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano hasa pale wanapokuwa wakitoa maelezo ya
awali,inapofika wakati wa kufikishana mahakamani wamekuwa wamekuwa wakikanusha
maelzo yao huku wengine wakisema kuwa wameandika maelezo kwa kitishiwa aidha
kwa silaha au vitu vingine.
Akizungumza
katika kikao cha kawaida cha Baraza la
Madiwani katika halmashauri ya mji wilayani Kahama,Mkuu wa Takukuru Mkoa
maalumu wa Kahama,Chrisantus Ndibaiukao alisema kuwa kesi inapofika mahakani mtoa
ushahidi amekuwa akikanusha ushahidi ambao alitoa nakuongeza kuwa ushahidi huo
ameutoa kwa kulazimishwa.
"Tumekuwa
tushindwa kesi nyingi kutokana na ushirikiano mdogo wawananchi kutoa ushahidi
hasa pale kesi zinapokuwa zimepelekwa mahakamani na wamekuwa wakikataa kile
ambayo kimeandikwa na wakisema kuwa wamelazimishwa kuandika ushahidi huo"
alisema.
Aidha
Ndibaiukao alitaja kesi ambazo zimeshafikishwa mahakamani ni tisa huku kesi
tatu zilitolewa maamuzi na walengwa walichukuliwa hatua za kisheria, nakuongeza
kuwa kesi nyingine tatu zilishindikana kutolewa ufafanuzi kutokana na
kutotolewa ushahidi vema toka kwa wananchi.
Hata
hivyo aliwataka wananchi wanatoa taarifa katika ofisi za takukuru juu ya
vitendo viovu vya rushwa kutoa ushirikiano hasa pale kesi inapofika mahakamani
nakuongeza kuwa hali hiyo itapelekea kushinda kwa kesi na sio kushindwa na
kukatia rufaa.