VITUO
vya afya vinavyomilikiwa na Watu binafsi,vimeaswa kufanya kazi kwa weledi na
kuzingatia taratibu na maadili ya sekta ya afya,na kuhakikisha wanatoa kodi zao
kwa wakati ili kuleta maendeleo kwa Taifa.
Aidha
vimetakiwa kuhakikisha vinatimiza wajibu kwa umma kadri vibali vyao
vinavyoelekeza na kuepuka vitendo vya utoaji mimba kwa jamii ,ambavyo vinakiuka sheria na utamaduni na wa
nchi kwa kulitia doa Taifa.
Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa Uhuru,George Mbijima,alitoa onyo hilo wakati akifungua
kituo cha Afya cha Kwema kilichopo Kata ya Nyasubi katika Halmashauri ya Mji wa
Kahama kinachomilikiwa na mtu binafsi,kwa
kuasa itoe huduma kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria za afya nchini.
Wamiliki
wa vituo vya Afya Binafsi Wilayani Kahama wametakiwa kuacha kujihusisha na
utoaji mimba kwenye vituo vyao kwani hali hiyo ni hatari na ni kinyume cha
taratibu ya vibari wanavyopewa na serikali kwa ajili ya kufanya shughuli za
kuhudumia wananchi.
Mbijima
alionya Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria wadau wa sekta
za Afya ambao wanakiuka utoaji huduma stahiki kwa wananchi kwa kushiriki tabia
za utoaji mimba kwa lengo la kujiongezea kipato,kwakuwa hayo hayakuwa malengo
ya serikali kutoa vibali kwa watu binafsi kumiliki vituo vya afya.
Alikumbusha
kuwa lengo la serikali kutoa vibali ni kusaidia huduma za Afya kwa wananchi,hivyo
ni vyema wakazingatia weledi wa taaluma hiyo sambamba na kuhakikisha wanalipa
kodi stahiki kwa wakati kwa ajili ya
maendeleo ya nchi,na kuhakikisha wanaajili watumishi wenye taaluma na kuwapatia
maslahi pasipo vikwazo.
Kiongozi
huyo wa mbio za mwenge,alitumia fursa hiyo kuwashawishi wanafunzi kupenda
masomo ya sayansi na kuyasoma kwa bidii kusudi wapate kusaidia kuondoa ombwe linaloikabili sekta ya afya nchini ya
ukosefu wa wauguzi na waganga.
Katika
taarifa yake Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Kwema Pauline Mathayo alisema
mradi huo uliogharimu Shilingi Milioni 578 utahudumia wananchi wanaozunguka
Kata ya Nyasubi wapatao 24,217 ambapo kati yake wanawake wenye umri wa kuzaa
Elfu tano mia tatu Ishirini.
Mathayo
alisema mbali na wanawake hao wajawazito pia kitahudumia idadi kama hiyo kwa
watoto wenye umri chini ya miaka mitano,ambapo pia kutakuwepo huduma kwa
wanachama wa Bima ya Afya ambapo wamejipanga kw kumudu kutoa huduma ya vipimo
vyote vya kisasa katika maisha ya binadamu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Fadhili Nkuru alimwambia kiongozi wa mbio za mwenge kwamba utatembele miradi tisa yenye thamani ya
Shilingi 1,891,708,722/- katika Halmashauri ya Mji,na baada ya hapo utakimbizwa
katika Halmashauri mbili za Msalala na Ushetu.