SERIKALI
ya awamu ya tano,imedhamiria kuifikisha nchi katika uchumi wa kati,ambao ni wa
viwanda,lakini dunia kuwa kijiji kimoja,kutokana na mabadiliko ya
teknolojia na uwepo wa
mitandao,inayotumiwa vibaya na vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa,inatishia
kuathiri uchumi wa taifa.
JAMII
imeaswa kubadilika kwa kuhakikisha inapambana kwa nguvu na mmomonyoko wa
maadili unaochagizwa na maendeleo ya teknolojia na utandawazi,kwa kuitumia
mitandao kwa faida ili kufanikisha nchi kuelekea katika uchumi wa kati.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Rocken Hill Academy,Alexander
Kazimil,inayomiliki shule za Msingi za Rocken Hill Academy na Rocken Hill
Junior pamoja na Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges,katika mahafari ya nane
ya kidato cha nne,ya sekondari yake kwa kuitaka jamii ishikamane kulinda
maadili ya nchi.
Kazimil
alisema wakati nchi ina mkakati wa kuelekea katika uchumi wa nchi,jamii itambue
vijana wengi wameathiriwa na matumizi ya mitandao,katika masuala ambayo hayana
tija zaidi ya kuharibu maadili ya Kitanzania, na kudai hali hiyo ikifumbiwa
macho italikwaza taifa kufikia malengo tarajiwa.
“Matumizi
ya mitandao kwa watoto imeathiri uwekezaji na utoaji elimu,kwani badala ya kujikita katika programu zenye tija,zitakazo
kuwa na faida kielimu na hapo badaye kusaidia kukuza uchumi wa nchi,wanajitumbikiza
kufuatilia mambo ya anasa,”alisema Kazimil.
Alisema
hivyo wazazi,walezi na jamii kwa ujumla
wanawajibu kuwa karibu na vijana
ambao ndio nguvu kazi ya Taifa,kwa kuwaelekeza,kuwashauri na kuwaonya juu ya
matumizi mabaya ya mitandao ili kujenga Taifa lenye maadili,hatua itakayosaidia
uwajibikaji uliotukuka na kufanikisha kufikia uchumi wa kati.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika mahafari hayo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Shinyanga,Muliro Muliro,alisema vijana hawana budi kutumia fursa ya muda kwa
kuhakikisha wanapata maarifa wanapokuwa shuleni,huku wakitumia mitandao
kujikita katika programu zitakazowapatia faida.
Kaonya
vijana kutumia muda mwingi katika mitandao katika masuala ambayo hayana faida
kiasi cha kuwatumbukiza katika masuala ya makosa mitandao,huku akiwasihi
wahitimu kuepuka kujiunga katika vikundi vya vijana wanaotumia madawa ya
kulevya,bali wakapambane na vitendo hivyo kwa faida ya nchi.
Awali
Mkuuwa Shule ya Sekondari ya Anderlek Ridges,Adamu Lui,aliitaka jamii
kushikamana katika suala la malezi, hatua itakayorejesha misingi bora ya
maadili ya Taifa inayoathiriwa na utandawazi,kwa kuwekeza katika elimu,na
kutambua wajibu wa kushirikiana na walimu katika maendeleo ya masomo kwa
mwanafunzi sambamba na kusimamia maadili ya Taifa.