SHIRIKA la World Vision Tanzania,limeomba wananchi na viongozi wa Halmashauri
ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, kutoa ushirikiano wa hali na mali katika
kutekeleza na kufanikisha mradi wake wa Afya na Lishe ya
Mama na Mtoto wilayani
Kahama.
Mradi
huo wa miaka minne na miezi sita, umelenga kuboresha lishe ya mama na mtoto
katika jamii ili kupunguza vifo utatekelezwa kwa
kushirikiana na Shirika la World Vision Canada na unafadhiliwa na Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya CANADA (Global Affrairs of Canada-GAC),Shaban Njia anaandika.
kushirikiana na Shirika la World Vision Canada na unafadhiliwa na Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya CANADA (Global Affrairs of Canada-GAC),Shaban Njia anaandika.
Akitambulisha mradi huo mbele ya kikao cha Baraza la Madiwani wa Halamshauri ya Mji wa Kahama jana,mjini Kahama,Mtaalam bingwa na Mshauri wa jinsia wa Shirika hilo Lutufyo Kaminyonge,alisema kuwa mradi huo unaotekelezwa kwenye Halmashauri tatu za Kahama Mji,Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga.
Akifafanua juu ya Mradi huo,Kaminyonge alisema kuwa mojawapo kati ya shughuli zitakazofanyika katika kipindi hicho ni katika kupunguza vifo vya mama na mtoto na ushawishi unaendana na utetezi katika usimamizi na maboresho ya Sera katika afya,lishe,kilimo na jinsia kuanzia ngazi ya msingi hadi serikali kuu.
Alisema katika bajeti,jumla ya dola za kimarekani 1.2 milioni sawa na takribani shilingi za kitanzania bilioni 2.6,zimetengwa kwa shughuli za moja kwa moja jamii katika vijiji 10 katika halmashauri ya wilaya ya Kahama.
Aliwataka
madiwani ambao ni wenyeviti wa Kamati za Maendeleo za Kata na wahamasishaji wa
wananchi katika fursa na shughuli mbalimbali za maendeleo kutoa ushirikiano wa
dhati kutekeleza mradi huo katika halmashauri hiyo.
Aliongeza kuwa katika Mradi huo wananchi kupitia mafunzo mbali mbali ya masuala ya lishe,jinsia,sera ya afya na lishe sambamba na mafunzo kwa wataalam wa afya ili kuinua uwezo wa kuwahudumia na kuwaelimisha wananchi masuala ya lishe.
Aidha alisema katika kufanikisha ndani ya jamii pia vikundi vya wakulima vitajengewa uwezo katika masula ya kilimo cha kuzalisha maza yenye wingi wa virutubisho na yaliyoboreshwa kibaologia(Nutrition Dense food and biofortified Crops)ikiwemo kulima viazi vya njano vinavyo daiwa kua ni vyenye virutubisho nyingi.
Kaminyonge alisema kuwa fursa nyingine katika Mradi huo ni Madiwani kushiriki katika majadiliano ya pamoja na serikali kwa kuwawakilisha wananchi kupitia Modeli ya World Vision ya sauti ya Umma(Citizen Voice and Action-CVA) yanayosaidia kuboresha huduma za jamii zinazogusa maisha ya kila siku kama afya,elimu na maji.
Pia alisema hayo yote yatafanyika kwa kutumia watalaam toka ndani ya halmashauri hiyo,Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii na Taasisi nyingine za serikali kama TFNC ambapo Mradi huo wa ENRICH toka World Vision utakuwa mratibu wa shughuli na uwezeshaji.
Mradi huo unaojulikana “Enhancing Nutrition Services to Improve Maternal and Child Health in Africa and Asia (ENRICH) unafanyika katika mikoa ya Shinyanga na Singida,umelenga kuwanufaisha jumla ya kina mama 381,698,wanaume200,689, wasichana 158,728 na wavulana 165,206 hapa nchini,kwa bajeti ya jumla ya dola za kimarekani 3.4 takriban sawa na shilingi za kitanzania bilioni 6.8. kwa kipindi cha miaka minne na miezi sita.
Vijiji vitakavyo nufaika na Mradi huo na kata zake katika mabano katika Halmashauri ya Mji wa Kahama ni Nyashimbi (Muhongolo) Nyandekwa (Nyandekwa) Kitwana (Busoka), Tulole (Kilago), na Inyema(Inyema).
Na Iponya (Kagongwa), Mpela (Isaghehe), Mondo (Penzi),
Mwendakulima(Mwendakulima) na Seeke(Zongomela).