TATIZO la watoto wa
mitaani,linazidi kushamiri nchini,huku kukiwa na jitihada hasi za serikali kuwakomboa,kutoka
katika madhila yanayowakabili katika maisha yao ya kila siku,yanaowakosesha
haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Hata hivyo,Kanisa katoliki jimbo la Kahama limeanza mikakati wa
ujenzi wa vituo viwili,vya kulea watoto hao wa mitaani pamoja na yatima,ili
kuhakikisha wanapata stahiki zao sambamba na kituo cha kulea wazee wasiojiweza,anaandika
Paschal Malulu.
Askofu wa jimbo Katoliki la Kahama,Ludovick Minde,alibainisha
mpangu huo,wakati wa misa maalumu ya kuwaombea watu wenye ulemavu mbalimbali,wakiwemo
albino walemavu wa macho,yatima na wazee
ambayo ilienda sambamba na kupata chakula pamoja.
Askofu Minde alisema Kanisa linatambua changamoto inayowakabili yatima,wazee
na watu wenye ulemavu wa viungo mbalimbali,na kuamua kuleta usaidizi kwa
kujenga vituo hivyo,kwa kuwaweka pamoja ili kumtambua Mwenyezi Mungu huku
wakipatiwa haki zao za msingi.
Alisema kwa kuwaweka pamoja watoto wa mitaani mbali ya kumjua
Mwenyezi Mungu,pia itasaidia kuwajenga kisaikolojia na kutambua umuhimu wa
elimu,ambayo ndiyo itakuwa msingi mkubwa wa maisha yao,ambapo alithibitisha
mpango huo kufanikishwa na mfuko wa jimbo hilo.
Aidha alifafanua kuwa kupitia mapadri kwa ujumla wataunga mkono
jitihada hizo na kuongeza kuwa ujenzi huo utaanza ndani ya mwaka huu kwani sasa
bado changamoto yakupata eneo ambalo litakuwa salama kwa watu hao ambao
watakuwa chini ya uangalizi wa jimbo la Kahama mjini.
Aliwasihi walemavu kukubaliana na changamoto wanazokumbana nazo ikiwa ni sambamba na wao kukubali msaada wanaopatiwa hata ikiwa kidogo kwani kukataa msaada huo ni kukiuka matakwa ya mungu kwani waumini wanatoa kile alichonacho.
Ibada hiyo ilifanyika ikiwa ni maadhimisho wa mwaka wa huruma,na
ikifanyika kwa mara ya kwanza katika jimbo hilo na kuwashiriksha watu wa kada
hizo na kukamilika kwa kupata chakula cha pamoja.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI