Thursday, April 28, 2016

WAZEE KAHAMA WAIOMBA SERIKALI IIVUNJE HALMASHAURI YA MJI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

UMOJA wa Wazee Wilaya ya KAHAMA(UWAKA)wameishauri Serikali ya Rais John Magufuli kulivunja Baraza la Madiwani la  Halmashauri ya Mji,kufuatia uelekeo wake kuonekana wa maslahi binafsi yasio na tija kwa umma.

UWAKA wametoa ushauri huo Siku chache tangu madiwani wa Halmashauri ya Mji kususa kuhudhuria mkutano wa had hara wa Mbunge wa Jumbo la Kahama Mini,Jumanne Kishimba,baada ya kutofautiana katika kikao cha baraza kuhusiana na gharama za matengenezo ya miundo mbinu ya barabara zilizopingwa na Mbunge huku madiwani wakishinikiza suala hilo liamriwe na Kamati ya Mipango Miji.

Wakiongea katika Kikao chao maalumu juzi ambacho kwa kauli moja kiliadhimia kuishauri serikali kulivunja baraza hilo ambalo limejipambanua lipo kwa maslahi binasfi si ya Umma.

Katibu wa UWAKA,Paul Ntelya alisema ushauri huo umezingatia maslahi mapana ya Kahama ambayo ina uchumi mzuri usiolingana na maendeleo kutokana na kuhujumiwa na watendaji wa serikali,halmashauri kwa kushirikiana na wanasiasa.

Ntelya alipongeza jitihada alizoanzisha Mbunge huyo zilizosaidia kufichua ufisadi katika Halmashauri na kusababisha kufukuzwa kazi kwa watumishi watano ambao hata hivyo wanashangazwa kutofikishwa mahakamani.

Alisema wanampongeza Mbunge kwa jitihada alizoanzisha kuibua na kukemea ubadhirifu katika Halmashauri ya Mji,ambako kumekuwa na matumizi yasiyozingatia uhalisia wa Huduma inayotolewa na kuwa sababu ya kutopatikana maendeleo stahiki.


"Kwakuwa madiwani hawako na Mbunge,tunaishauri mamlaka inayohusika ivunje baraza na kuunda Kamati itakayoshirikiana na Mbunge kuleta maendleo,"alisema Ntelya.

Nae Mzee Hassain Kaghoma mkazi wa Kata ya Majengo alisikitishwa na madiwani wanaounda halmashauri hiyo ambao wote kasoro mmoja wanatokana na CCM ambao walikuwa na matumaini nao kuleta maendeleo kwa kudhani awamu iliyopita walikwamishwa na wenzao wa upinzani.

"Kuna usemi,ndege wa rangi moja huruka pamoja awamu iliyopita kulikuwemo na madiwani wa upinzani tulidhani ni kikwazo kwa maendeleo,kumbe hata maendeleo kidogo yaliyopatikana awamu iliyopita wanatuaminisha ni jitihada za wapinzani maana wengi wa madiwani ni walewale wa awamu iliyopita na ndio wanaompinga mbunge,bora baraza lao livunjwe,"alisema Mzee Kaghoma.

Kwa upande wake Mzee Balthromew Kayoka,mkazi wa Kata ya Nyasubi,alisema mdudu alioingia katika baraza hilo tiba yake ni kuvunjwa na kuwepo kwa Kamati kwani kwa upinzani waliouonesha wamedhihirisha ndio kikwazo cha maendeleo kutokana na kuaminiwa na wananchi kwa miaka mingi huku kukikosekana maendeleo stahiki.

Alisema na kwakuwa wameonesha kusigana na Mbunge hadi kususa kuhudhuria mkutano wake,ni budi serikali ikatengua uwakilishi wao na kuunda kamati vinginevyo Kahama hapatapatikana maendeleo kwa miaka mitano kutokana na masigano ya wanasiasa huwa endelevu huku wakihadaa umma kuwa hawna ugomvi.

Mwaka 1997 Rais wa awamu ya tatu,Benjamin Mkapa alitishia kuvunja Halmashauri ya Wilaya ya Kahama kwa madai kuwepo kwa mchwa anayetafuna pesa za miradi ya Maendeleo ya Kahama.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI