Monday, April 11, 2016

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI KIKAANGONI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



WAKURUGENZI wa Halmashauri za Majiji,Manispaa,Miji na Wilaya nchini wametakiwa kutenga asilimia kumi za mapato katika Halmashauri wanazoziongoza kwa ajili ya wanawake na vijana vinginevyo atakayeshindwa ataondolewa.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Majaliwa Kassimu Majaliwa,katika mkutano wa hadhara vijiji vya Kitandi,Mtimbo,Likunja,Nkowe na Namahema wilaya ya Ruangwa,Mkoani Lindi,ambapo amezitaka kuhakikisha asilimia hiyo zinawafikia walengwa hao.

Waziri Mkuu ambaye yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo alisema suala la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi ni la lazima.

“Suala hili ni lazima si hiari,Halmashauri ambayo itashindwa kutenga asilimia tano kwa ajili ya vijana na tano kwa ajili ya akinamama Mkurugenzi wake atakuwa anatafuta safariiri,” alisema Waziri Mkuu, Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu aliwasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo kwa uadirifu  na serikali haitamvumilia yeyote atakayeshindwa.

Pia Waziri Mkuu, Majaliwa aliwataka wananchi hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili zitakapofika sh milioni 50 za kila kijiji zilizoahidiwa na Rais, Dk. John Magufuli waweze kunufaika.

Alisema fedha hizo ambazo
 zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa katika vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja hivyo amewataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa alisema serikali imefuta tozo tano kati ya tisa za zao la korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya wakulima wachukie mfumo wa Stakabadhi ghalani.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI