RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa mkoa
huo,kwa kinachodaiwa kutoa taarifa za uongo kuwa hakuna watumishi hewa
mkoani kwake.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zinaeleza kwamba Anne Kilango alimhakikishia rais kwamba mkoani kwake hakuna watumishi hewa ilhali wapo.
Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anne Kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zinaeleza kwamba Anne Kilango alimhakikishia rais kwamba mkoani kwake hakuna watumishi hewa ilhali wapo.
Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anne Kilango Malecela kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa.
WAKAZI wa Mkoa wa Shinyanga walimtawaza kuwa Chief ama Mgole wa Wasukuma mara aliporipoti na kuanza kufanya kazi mkoani humo. |
Baada
ya taarifa hizo, rais Magufuli aliamua kutuma jopo watu maalum kutoka Ikulu kwa
ajili ya kufanya uchunguzi huo na kugundua kuwa kuna idadi ya watumishi hewa 45
katika mkoa huo.
Imeelezwa jopo hilo kutoka
Ikulu,limefanya uchunguzi wake na
kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili
ya uchunguzi bado inaendelea.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam
wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge
baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza
kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa huo,Abdul
Dachi,kuondolewa ofisini mara moja.
![]() |
ANNE Kilango Malecela siku alipokula kiapo cha kutumikia Ukuu wa Mkoa. |
Anne Kilango Malecela,aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Malecela,kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Machi 13,2016 na kudumu katika wadhifa huo kwa muda wa siku 30,huku akiwa Mkuu wa Mkoa wa 19 na wa kwanza mwanamke katika Mkoa wa Shinyanga.
Wakati akiwaapisha Wakuu hao wa mikoa,Rais Dkt.Magufuli, aliwapatia siku 15 kubaini watumishi hewa katika maeneo yao ya kazi,ambapo muda huo ulipotimia Mkoa wa Shinyanga ulitangaza kutokuwa na mtumishi hewa hata mmoja.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI