Monday, April 11, 2016

JPM KUFANYA ZIARA UGHAIBUNI NA MSAFARA WA WATU KUMI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




BAADA ya ziara ya nchini Rwanda,Rais John Magufuli anataraji kusafiri nje ya nchi, hivi karibuni,huku ikielezwa  msafara wake kuna uwezekano mkubwa ukawa na watu wasiozidi kumi.

Imeelezwa idadi hiyo ndogo ya watu inatokana na falsafa za Rais Dkt,Magufuli za kubana matumizi,ikiwa ni siku chche tangu alipotumia siku 153 tangu kuapishwa kwake kufanya ziara ya kwanza ya nje ya nchi,kwa kuzuru nchini Rwanda kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame Jumanne iliyopita.

Rais alikwenda Rwanda kwa ajili ya kufungua daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha biashara chenye huduma za pamoja, ambacho ni kiunganishi muhimu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Ambapo msafara wake ulikuwa na watu wasiozidi kumi.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga, alisema jana kuwa Rais Magufuli anatarajia kusafiri tena kwenda nje ya nchi hivi karibuni.

Balozi Mahiga alisema katika safari hiyo, msafara wake utaendelea kuhusisha watu wachache wenye umuhimu katika safari husika ili kuepukana na gharama zisizokuwa za lazima.

Hata hivyo, Balozi hakutaja nchi hiyo itakayofuatia baada ya ziara ya Rwanda wala siku ya kusafiri.Japo alisisitiza ziara za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ndani na nje ya nchi zitazingatia watu wachache wenye umuhimu katika ziara hizo.

Akiwa Rwanda, Rais Magufuli alisema hapendi kusafiri kwenda ughaibuni kwa sababu anapenda kubana matumizi kwa vitendo.

Akizungumzia kauli hiyo, Mahiga alisema ni kweli, mara zote Rais Magufuli amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kila mmoja ndani ya serikali yake kubana matumizi yasiyokuwa ya lazima na ndiyo maana amekuwa akilidhihirisha hilo kwa vitendo.

“Rais anachosema kuhusu kubana matumizi ni kweli kabisa… ndiyo maana msafara wake katika ziara hiyo (ya Rwanda) hatukuzidi watu kumi. "Hii inamaanisha hataki kuwapo kwa matumizi makubwa katika safari za nje.”

Aidha, Balozi Mahiga alifafanua kuwa baadhi ya mawaziri na maafisa wengine kadhaa walioshiriki shughuli ya uzinduzi wa daraja la Rusumo waliishia hapo na kurudi wakati yeye na maafisa wachache wa serikali wakiongozana na Rais katika ziara ya Rwanda.

“Nafikiri mliwaona baadhi ya mawaziri pale Rusumo… wale walitokea huku Tanzania na kurudi. Hawakuwamo katika msafara uliokuwa Rwanda,” alisema Balozi Mahiga.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI