KESHO Wafanyakazi wote
nchini wanaungana na wenzao Duniani,kuadhimisha siku yao,huku Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA)likihitaji kima cha chini cha mshahara wa
mfanyakazi wa umma kiwe Sh.750,000/-na kisikatwe kodi.
Katibu Mkuu wa
TUCTA,Nicholaus Mgaya,amesema Utawala wa awamu ya tano chini ya Dkt.Magufuli,uliwaahidi
mabadiliko wafanyakazi,hivyo nao wanahitaji mabadiliko yanayolenga kuboresha
maisha yao.
TUCTA imepata kuingia
katika mgogoro mkubwa na Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu Jakaya
Kikwete,walipotishia kugoma wakishinikiza kima cha chini cha mshahara kiwe
Sh.315,000/-.
Hata hivyo mgomo huo
haukufanikiwa baada ya Kikwete kuweka wazi kuwa Serikali haina uwezo huo na
kuwataka wafanyakazi wasikubali ushawishi wa Mgaya,bali akiwaambia akili za
kuambiwa wachanganye na zao.
Hadi Awamu ya nne
ikimaliza muda wake imeacha kima cha chini cha Mshahara Sh.240,000/ kwa mfanyakazi wa sekta ya Umma,ambacho
anaendelea kulipwa Mtumishi wa kada hiyo.
Mgaya ameitaka Serikali ya
Awamu ya Tano,kuongeza nguvu katika kupunguza matatizo mengi yanayowakabili
wafanyakazi ikiwemo mishahara midogo isiyoendana na gharama za maisha.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI