JAPOKUWA Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli,hakuutaja mkataba husika,lakini
kitendo cha kulitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa zinazosemwa,ni kana
kwamba amejitosa kwenye kashfa za ufisadi unaozungumzwa kufanyika baina ya
Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd.
Rais Dkt.Magufuli akiongea
jana mkoani Dodoma kwenye kikao kazi,cha makamanda wa polisi wa mikoa,mawakili
wafawidhi wa mikoa na wakuu wa upelelezi wa mikoa na vikosi,alisema mikataba ya
ovyo iliyoingiwa imelidhalilisha jeshi hilo,huku akiitaka ofisi ya Mwendesha
Mashitaka na Polisi kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia
maslahi ya Taifa.
Kampuni ya Lugumi
Enterprises Ltd na Jeshi la Polisi nchini walitiliana saini mwaka 2011 kwa
ajili ya kufunga vifaa vya kuhifadhi alama za vidole 108,katika vituo vya
polisi na kuzua gumzo kwa kipindi hiki hapa nchini.
Utata wa Mkataba huo
umeifanya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC),kuunda Kamati
ndogo ya kufuatilia.
![]() |
RAIS John Magufuri akiongea na Makamanda wa Polisi wa Mikoa. |
Makubaliano ya Mkataba huo
yalikuwa ni Kampuni ya Lugumi ifunge vifaa hivyo 108 katika vituo vya Polisi
kwa gharama za Shilingi Bilioni 37,lakini mpaka sasa inadaiwa ni vifaa 14
vilivyofungwa huku Kampuni hiyo ikiwa tayari imeishalipwa asilimia 99 ya malipo
ambazo ni Sh.Bilioni 34.
Kuna madai utekelezaji wa
mkataba huo tata uliozua mijadala kila kona nchini umewahusisha vigogo wa
serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani,Charles Kitwanga na Mkuu wa Jeshi la
Polisi Mstaafu,Said Mwema,wanaodaiwa kuhusika.