MAMLAKA ya Hali ya Hewa
Tanzania(TMA),imetoa tahadhari katika mikoa ya Ukanda wa Pwani na Visiwani
Zanzibar,kwamba mvua kubwa inatarajiwa kunyesha kuanzia April 26 hadi 29,mwaka
huu,na kwamba inaweza kusababisha mafuriko.
Taarifa kutoka TMA
inaeleza kunyesha kwa mvua kubwa yenye kiwango cha milimita 50 ndani ya saa
Ishirini na nne,ambayo itaambatana na upepo mkali unaozidi kasi ya Kilomita 40
kwa saa na mawimbi yasiyozidi mita 2.0.
Taarifa hiyo inabainisha
kiwango cha uhakika ni asilimia 80 itakayonyesha katika mikoa ya Tanga,Dar Es
Salaam,Mtwara,Pwani,Lindi,Morogoro na Visiwa vya Pemba na Unguja.
Pia mvua hizo zinatarajia
kusambaa katika maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro na mashariki mwa Manyara.
Taarifa hiyo ilieleza
kwamba mvua hiyo inatokana na kuwepo kwa mgandamizo mdogo wa hewa katika pwani
ya Tanzania unatokana na kilichokuwa kimbunga aina ya Fantala.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI