THOMAS Barasa amehukumiwa
kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kichaa,Samuel Njoroge,ili
kutimiza matakwa ya ushirikina kujipatia utajiri.
Hakimu Ngenye Macharia wa
Mahakama Kuu ya Eldoret,ya Jijini Nairobi,alitoa hukumu hiyo jana baada ya
kuridhika na upande wa mashahidi,baada ya kesi hiyo kuunguruma kwa kipindi cha
miaka mitano.
Kulingana na ushahidi
ambao uliwasilishwa mahakamani hapo,mshukiwa alitenda unyama huo kwa
kushirikiana na watu wengine ambao hawakuwa mahakamani,baada ya kushawishiwa na
mganga aliyetajwa kwa jina moja la Omonding wa eneo la Mpakani,atafute viungo
vya mwili wa binadamu kwa ahadi ya malipo ya Sh.500,000.
Inadaiwa kuwa Barasa na
wenzake walitumia pombe aina ya Chang’aa,kama kivutio cha kumnasa marehemu
aliyekuwa na tatizo la akiri.
Ushahidi uliowasilishwa
ulionyesha kuwa Barasa kwa kushirikiana na wenzake walimuua na kumkatakata
Njoroge baada ya kumlewesha chang’aa,kisha kutupa mwili wake katika shimo
ambalo lilikuwa kando ya nyumba ya mshukiwa,Septemba 4,2010.