
SERIKALI
imewataka Watanzania kufunga mkanda kuanzia mwaka ujao wa fedha kusudi malengo yaliyopo ya kuitoa nchi katika umaskini yaweze kutimia.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa fedha na mipango, Mhe Dkt Phillip Mpango,wakati akiwasilisha bungeni mpango wa pili wa maendeleo ya taifa kwa mwaka fedha 2016/17 hadi 2020/21.
Amesema katika mwaka wa
fedha ujao ili kufikia azma hiyo serikali imepanga kutumia asilimia 40
ya mapato yake katika miradi ya maendeleo ambapo amewataka watanzania
kubadilika kujenga tabia ya kulipa kodi.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu mpango wa pili wa maendeleo ya taifa wabunge wamekuwa na mitazamo tofauti ambapo baadhi wameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuja na mpango wa unaoangalia maeneo muhimu katika ukuaji wa uchumi, huku wakionyesha kutoridhishwa na mpango huo.
Aidha baadhi ya wabunge wamewataka wabunge kuanza kujadili vyanzo vya mapato vitakavyoweza utekelezaji wa mpango huo, huku wengine wakisisitiza kutokufanya hivyo kutarejesha yaliyofanyika katika mpango wa kwanza wa maendeleo ambapo mbaka sasa utekelezaji wake inaamika haujafikia zaisi ya asilimia 60