Thursday, April 21, 2016

YANGA YAANGUKIA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



TIMU za Ukanda wa Afrika Mashariki zimeendelea kuwa vibonde kwa timu za kanda ya Kaskazini ya Afrika,baada ya Wawakilishi wa Tanzania,Yanga African kukubali kipigo cha bao 2 -1 katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na kuaga michuano hiyo.
 
Yanga imekubali kipigo hicho ikiwa ni siku moja baada ya kutolewa kwa klabu ya Azam FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na klabu ya Esperance ya Tunisia, macho ya watanzania April 20 2016 yalielekezwa katika mchezo kati ya Yanga wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Yanga ambao mchezo wa awali uliochezwa Taifa Dar es Salaam walimaliza kwa sare ya goli 1-1, walienda Misri katika mji wa Alexandria kutafuta sare ya goli 2-2 ili waweze kufuzu au washinde mchezo huo kwa bahati mbaya Yanga wamekubali kipigo cha goli 2-1.
Klabu ya Al Ahly ya Misri ndiyo walianza kupata goli la uongozi kipindi cha pili, lakini Yanga walisawazisha dakika ya 57 kupitia kwa Donald Ngoma aliyetumia vyema krosi ya Juma Abdul, mambo yalizidi kubadilika zaidi kuanzia dakika ya 80 baada ya Al Ahly kuongeza nguvu ya kuishambulia kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la ushindi dakika ya 95.
Kwa matokeo hayo Yanga wanakuwa wamerejea rekodi yao ya kufungwa na Al Ahly ya Misri, ambayo mwaka 2014 walifungwa tena katika hatua ya mikwaju ya penati 5-4 kwa nne. Yanga kwa sasa wanarudi kushiriki Kombe la shirikisho barani Afrika.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI