MAMLAKA
ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar, ambayo ina majukumu
sawa na Takukuru ya Bara, imepanga kumhoji Makamo wa Kwanza wa Rais
mstaafu, Maalim Seif Sharif Hamad.
Maalim
Seif atahojiwa na taasisi hiyo kufuatia madai aliyotoa hivi karibuni
kuwa kuna viongozi wa Serilai ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wanamiliki
fedha chafu nje ya nchi.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Mussa Ali,
alisema watamhoji kiongozi wa upinzani na Katibu Mkuu huyo wa Chama cha
Wananchi (CUF), ili kusaidia uchunguzi dhidi ya madai yake.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI
Amesema wanataka awasaidie taarifa za vigogo hao wanaomiliki fedha chafu nje ya nchi ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Anasema;“Tumeunda
timu maalum ya kuchunguza tuhuma kama hizo kwa madhumuni ya kuchukua
hatua za kisheria pale tunapopata ushahidi wa kutosha hivyo tutamhoji
Maalim Seif,”
Maalim
Seif alitoa kauli hiyo kuwa kuna viongozi wengi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambao wameficha fedha chafu nje
ya nchi.
Alizitaka Jumuiya za Kimataifa kufuatilia akaunti za viongozi hao nje na kuwachukulia hatua za kisheria.
Madai
ya Maalim Seif yalikuja katika kipindi ambacho dunia imegubikwa na
kashfa ya 'Nyaraka za Panama' ambapo viongozi mbalimbali mashuhuri
duniani, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon wamegundulika
kuficha fedha kwenye nchi hiyo ya Panama.
Waziri
Mkuu wa Iceland, Sigmundur Gunnlaugsson alijiuzulu nafasi hiyo Aprili 5
kutokana na maandamano ya kumtaka awajibike baada ya jina lake kuwa
mmoja wa watu waluioficha fedha Panama.
Wengine mashuhuri waliotajwa kwenye kashfa hiyo ni pamoja na wasaidizi wa karibu wa Rais wa Russia, Vladmir Putin.
Maalim
hakutaja majina ya viongozi hao lakini alisema suala la kuwepo vigogo
walioficha fedha nje ya Zanzibar halitaji tochi kwa sababu wengine
wanamiliki nyumba za kifahari Dubai kwa fedha walizopata kinyume na
sheria.
Wakati
huo huo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imemtaka Maalim Seif
kutaja majina ya vigogo anaodai wameficha fedha chafu nje ya nchi.
Akizungumza
jana mjini hapa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed
Aboud Mohamed alisema serikali ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein
itawachukulia hatua za kisheria endapo atawataja.
Maalim
Seif alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa
Kitaifa (SUK), lakini CUF ilisusia Uchaguzi Mkuu wa marudio wa Machi 20
na huivyo Katibu Mkuu huyo kupoteza nafasi yake.
CUF
ilisusia Uchaguzi Mkuu wa marudio ikidai ilipokwa ushindi katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar, Jecha Salum Jecha ambaye alitangaza kuufuta licha ya
waangalizi wa ndani na kimataifa kudai ulikuwa huru na wa haki.
ABoud
alisema serikali imedhamiria kupambana na vitendo vya rushwa, ufisadi
na kuimarisha misingi ya uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma.
Alisema
serikali imekusudia kuendelea kuimarisha dhana ya utawala bora na hatua
ya kuwataja majina viongozi walioficha fedha nje ya nchi itasadia
sheria kufuata mkondo wake.
“Maalim
Seif kama ana ushahidi awataje majina viongozi anaodai wameficha fedha
nje ya nchi, akifanya hivyo atakua amesadia serikali na vyombo vyake vya
sheria,” alisema Waziri Aboud.