NDOTO za vijana wa Msimbazi,za msimu huu kuwapa faraja mashabiki wake kwa kutwaa Ubingwa baada ya kuukosa kwa kipindi kirefu zimeyeyuka baada ya kukubali kichapo cha bao 1 - 0 kutoka kwa vijana machachari wa Toto African kutoka Jijini Mwanza.
Toto African ambao katika medani za soka hapa nchini wanafahamika kuwa na Udugu na mabingwa watetezi,Yanga African,imemudu kufuta ndoto hizo kwa kuibuka na ushindi huo huku ikutumia
baadhi ya wachezaji chipukizi na wenye vipaji waliowahi kuwika na Simba.
Baadhi ya waachezaji hao ambao walikuzwa na Simba kisha kuwatosa katika mazingira ya kutatanisha ni Edward Christopher, Hassan Khatib na Abdallah Seseme,ambao katika mchezo huo walikuwa mwiba mkali kwa kuweza
kucheza vema na kuisaidia Toto kuibuka na ushindi huo.
Goli
pekee la wanakishamapanda Toto Africans limefungwa kunako dakika ya 20
na mfungaji hatari wa timu hiyo kwa sasa Waziri Junior baada ya kupiga
shuti kali nje ya 18 lililomshinda kipa mu-Ivory Coast Vicent Agban na
kujaa wavuni moja kwa moja na kuipa alama tatu muhimu timu ya Toto
ambayo sasa imefikisha alama 30 kwa michezo 27.
Simba
ambayo imekuwa ikipata tabu mara kwa mara kwa misimu kadhaa kila
inapokutana na vijana hao wa Toto ambao kwa sasa wananolewa na kocha
John Tegete akisaidiwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake
Twiga Stars Rogasian Kaijage ilishuhudia kocha wake Mganda Jackson
Mayanja akitolewa nje kwenye benchi na mwamuzi Ahmada.
Mayanja almaarufu kwa jina la mia mia,alitolewa kwenye benchi la ufundi baada ya kuonekana kupishana kauli na mwamuzi huyo, hivyo Simba ikawa chini ya uangalizi wa
kocha wa Makipa Adam Abdallah.
Pigo
lingine kwa Simba lilikuwa mwanzoni mwa kipindi cha pili pale
iliposhuhudia beki wake kisiki wa upande wa kulia Hassan Kessy akipewa
kadi nyekundu na hivyo kuivuruga kabisa timu hiyo ambayo hii leo ilikosa
kabisa mbinu mbadala za kuipenya ngome ngumu iliyocheza kwa nidhamu
kubwa dakika zote za mchezo huo ikiongozwa na beki kisiki wa kati Hassan
Khatib aliyewahi kuwika na Simba kabla ya kutupiwa virago msimu huu
mwanzoni.
Kessy
ambaye hii leo alianza vema mchezo huo huku akipandisha mashambulizi
kwa kasi mara kwa mara katika lango la Toto alitolewa nje baada ya
kumchezea faulo mbaya, mshambuliaji kinda wa zamani wa Simba Edward
Christopher kunako dakika ya 2 kipini cha pili.
Matokeo
haya yanaifanya Simba ambayo inahaha kusaka nafasi ya ushiriki michuano
ya kimataifa msimu ujao kubaki katika nafasi ya pili kwa alama zao 57
mbili nyuma ya vinara Yanga ambao wako nyuma kwa mchezo mmoja huku Simba
wakifikisha michezo 25.
Kwa
misimu kadhaa sasa timu ya soka ya Simba imekuwa ikipata shida kila
inapovaana na timu ya soka ya Toto Africans ya Mwanza katika michuano ya
ligi kuu ya soka Tanzania bara VPL ikishuhudiwa Simba ikipotea ama
kuambulia sare mbele ya timu hiyo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI