Sunday, April 17, 2016

YANGA YAREJEA KILELENI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

BAO la mnamo dakika ya 46 ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara,limeiwezesha timu ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Mtibwa Sugar,hivyo kurejea kushika usukani mwa ligi hiyo.

Bao hilo lilowashusha kileleni mwa Ligi hiyo timu ya Simba,katika mchezo wa kiporo uliochezwa Jijini Dar Es Salaam,lilipachikwa mnamo Dakika ya 46, na Simon Msuva baada ya kupokea pande zuri la mpira wa faulo,iliyopigwa na Haruna Niyonzima.


Kwa ushindi huo Yanga inaongoza Ligi kwa kumudu kufikisha pointi ikiwa imebakiza michezo sita sawa na watani zake Simba ambao wanashika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kwakuwa na pointi


Katika pambano hilo ambalo kutokana na mvua ambayo ilinyesha jijini Dar es Salaam, uwanja ulikuwa na maji mengi na kusababisha baadhi ya wachezaji kuteleza na kupoteza kontroo.Vikosi vya timu vilikuwa;
 Yanga:
1. Deogratius Munishi ‘Dida’
2. Juma Abdul
3. Oscar Joshua
4. Kelvin Yondan
5. Nadir Haroub ‘Cannavaro’
6. Vicent Bossou
7. Simon Msuva
8. Thaban Kamusoko
9. Donald Ngoma
10. Haruna Niyonzima
11. Deus Kaseke/Amiss Tambwe(76)  na
Mtibwa Sugar:
1. Said Mohammed
2. Ally Shomari
3. Majaliwa Shabaan
4. Andrew Vicent
5. Salim Mbonde
6. Shaban Nditi
7. Shiza Kichuya/Vicent Barnabas(76)
8. Muzamiru Yassin
9. Seleman Rajab
10. Ibrahim Rajab/Henry Joseph(52).
11. Kelvin Friday

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI