MWANAKIJIJI Sibitali Nsumba akitoa maelezo kwa Mbunge. |
BAADHI ya wananchi katika kijiji cha
Isanga,Kata ya Idahina,Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama,wameukataa mradi
wa bwawa la maji uliokuwa ukitolewa msaada kutoka nchini Uingereza kupitia
Shirika la Oxfam.
Badiliko la kuukata mradi huo ambao
awali waliuafiki,lilianza kuwasilishwa na Sibitali Nsumba,alipodai Katika Kikao
chao na Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Elias Kwandikwa,kuwa pamoja na kwamba
alijitolea hekari tano kwenye shamba lake la Mpunga, ili bwawa hilo
lichimbwe,lakini ameahirisha.
Nsumba alisema katika kikao chao cha
kwanza aliafiki na kuwa ridhaa kutoa eneo lake hilo,lakini baada ya kugundua
kulikuwa na udanganyifu wakati wa kupitisha mradi huo,hayuko tayari kutoa
kuridhia eneo lake kutumika tena katika mradi huo.
MBUNGE wa Jimbo la Ushetu,Elias Kwandikwa akitoa ushauri. |
Alisema wakati wa Kikao cha Kwanza
cha kupitisha Mradi huo,utakaogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 150,walielezwa
kwamba ungeweza kutumia hekari tano tu, lakini baada ya upembuzi yakinifu
kufanyika, bwawa hilo lingeweza kutumia zaidi ya Hekari 15.
Kufuatia hali hiyo,Nsumba alisema
kama serikali itakubali masharti yake, bwawa hilo lichimbwe lakini iwe mali
yake binafsi, kuliko kuchimba kwa manufaa ya Kijiji, hivyo alimuambia Mbunge
huyo, hatoi tena eneo hilo na mradi huo wauondoe kwenye kijiji hicho.
Kauli hiyo iliungwa mkono na
wanakijiji wenzake, ambapo Saambili Lukubanija,alisema pamoja na kwamba
mradi huo ulipitishwa lakini jamii nyingi haikushirikishwa,hivyo na yeye
aliungana na Nsumba, kuitaka serikali iuondoe mradi huo kwenye kijiji hicho.
Kabla ya hapo, Diwani wa kata
hiyo,Yuda Majonjo,alisema wananchi hao walipitisha mradi huo wa bwawa ujengwe
kwenye kijiji hicho, na tayari fedha zimeishaingizwa, hali ambayo alidai hata
naye inamshangaza kwa wananchi hao kukataa mradi huo.
MBUNGE Kwandikwa akitoa ushauri katika eneo la Nsumba. |
Majonjo alisema, wananchi hao
waliupitisha mradi huo kwa taratibu zote za sheria za vijiji kwenye Mkutano, na
kuongeza kwamba baada ya hapo waliingia wanasheria wa mitaani ambao
waliwapotosha wananchi hao, hali iliyosababisha kukatawaliwa kwa mradi huo.
Nae Mbunge wa Jimbo la
Ushetu,Kwandikwa,alisema hawezi kuwalazimisha wananchi wa kijiji hicho, kupokea
mradi huo isipokuwa aliwataka wakatae kwa kufuata taratibu zote za Serikali ya
Kijiji, ikiwa na pamoja na kuitisha Mkutano Mkuu ili wananchi waweze
kushirikishwa.
“Kama mmedhamiria kuukataa mradi
huu,sintoweza kukulazimeshini,isipokuwa nakuombeni basi mfuate taratibu kama za
awali wakati mnauafiki,itisheni Mkutano Mkuu wa Kijiji, kisha muandike
muhtasari ukiwa ni pamoja na mahudhurio yote kisha tuupeleke sehemu husika kama
tulivyopeleka wakati wa kuupokea mradi huo,”alisema Kwandikwa.
Mradi huo wa bwawa ulikuwa
umeandaliwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la OXFAM,kwa
lengo la kutumika kwenye kilimo cha Umwagiliaji na tayari katika maeneo mengine
wilayani Kahama,mradi huo umepokelewa na utekelezaji wake umeishaanza.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI