MTOTO wa Waziri
Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary amewaomba radhi Watanzania kwa
kauli yake kwamba Olduvai Gorge iko nchini humo.
Maudhi hayo
yalisababisha kuibuka kwa mijadala katika mitandao ya Kijamii,kwa Watanzania
kujitokeza kumshutumu mtoto huyo wa Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa hilo la
Kenya.
Rosemary Odinga anasema
“Nilikosea,nawaomba radhi Watanzania,ukweli Bonde la Oldupai ama Olduvai liko
Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi
wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young
Leaders Assembly).”
Anaendelea kusema “Nahisi kama ambaye nimewakosea
ndugu zangu kutoka Tanzania.Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo
nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile
eneo la Kajiado.”
“Nahisi kama
ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania.Nisemeje ,,nawaombeni radhi
Watanzania.Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na Kenya.
‘Katika ile hali
ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika
mashariki ndio kitovu cha ubinadamu” alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa
Instagram.
Tamko lake
kuhusiana na bonde hilo la Olduvai (Oldupai) lililoko Tanzania lilihusiana na
mada ya siku hiyo.
‘Katika ile hali
ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika Mashariki
ndio kitovu cha ubinadamu” alisema bi Odinga
Olduvai ndiko
kulikopatikana vifaa vilivyotumika na watangulizi wa binadamu yapata miaka
milioni moja na laki sita iliyopita (milioni 1.6)
Bi Rosemary
aliomba radhi baada ya kuzomewa na maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii ya
Facebook Instagram na Twitter wakidai aliwapotosha hadhira yake na haswa
ulimwengu kwa kusema eti Olduvai ipo Kenya.
Kwa upande wake,Mbunge Zitto Kabwe
alikuwa amechangia mada kwa kusema kuwa Tanzania sharti izinadi vivutio vyake
vya kitalii ilikuzima dhana potovu.
Aidha alidai kuwa
watu wanafikiria kuwa mlima Kilimanjaro uko Kenya ilhali ukweli halisi upo
Tanzania sawa na mwanamuziki nyota Diamond Platnumz ambaye ni Mtanzania.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI